Wednesday, October 17, 2012

MAKAMU WA RAIS AOMBOLEZA KIFO CHA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo  ya msiba wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Ukonga jijini Dar es Salaam, kushiriki katika shughuli  za msiba huo na kutoa heshima za mwisho.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Ukonga jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, marehemu,  Liberatus Barlow.


MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA UJUMBE KATIKA OFISI YA BALOZI WA MAREKANI HAPA NCHINI



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Mwakilishi wa Biashara katika Ofisi ya Rais wa Marekani, Mhe. Balozi Demetrios Marantis, aliyefuatana na ujumbe wake, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo .


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwakilishi wa Biashara katika Ofisi ya Rais wa Marekani, Mhe. Balozi Demetrios Marantis, aliyefuatana na ujumbe wake, baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, Kulia ni Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Naibu Mwakilishi wa Biashara katika Ofisi ya Rais wa Marekani, Mhe. Balozi Demetrios Marantis, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwakilishi wa Biashara katika Ofisi ya Rais wa Marekani, Mhe. Balozi Demetrios Marantis, aliyefuatana na ujumbe wake, baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Tuesday, October 16, 2012

MKUTANO WA KUHAMASISHA UTALII WAFUNGULIWA




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia alipofungua Mkutano wa kwanza wa  Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. 

Mkutano huo umefunguliwa leo Oktoba 15, 2012 katika Ukumbi wa AICC  leo Oktoba 15 Jijini Arusha na kuhudhuriwa na mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Picha na OMR



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokea barua ya wazi kutoka kwa Katibu wa Mkuu wa Shirika la Utalii la Dunia, Taleb Rifai, iliyotolewa na Baraza la Waendesha Utalii Duniani (WTTC) mara baada ya kufungua Mkutano wa Kuhamasisha utalii barani Afrika leo, Oktoba 15, 2012, jijini Arusha. Katika Mkutano huo pia umehudhuriwa na Mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.Picha na OMR


                                        Makabidhiano yamekamilika