Friday, August 31, 2012

R.I.P HAWA NGULUME


                                               Hawa Ngulume enzi za uhai wake.


Bi Hawa Ngulume, aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Bagamoyo na Mbarali, amefariki dunia jijini Dar es Salaam. Mama Ngulume amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa kwa kipindi kirefu na mauti yamemfika akiwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar.
Kwa kujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana taratibu za mazishi  na maziko  zinaandaliwa na taarifa kamili itatolewa.
Mungu ailaze roho ya marehemu HAWA NGULUME  mahali pema peponi. AMINA

Thursday, August 30, 2012

Chriss Brown a.k.a Brezzy anayemchanganya Rihanna


Kiukweli huyu kaka anavutia unapomtazama, muoene alivyo amependeza mno! acha Rihanna aendelee kumkumbuka tu! he's good!


                         mwenzangu ukipendeza lazima swaggar uitupie pale kati! si unaona!?



si unaona kijana alivyo tupiamo? vijana wa kibongo na hasa mlioko kwenye music industry mupoo? thanx to Martin Kadinda model wa ukweli alowaletea single burton, angalau! mwapendeza yakeheeee! sio mbaya ukimuiga brizzy!



shughuli inaanzia hapa! wabunifu wa mavazi wanaweza wakakufanya uonekane kituko sometimes kiukweli! na hasa usipokua makini,juu ya nini unakubali kuvaa kwasababu wewe ni super star! we twende tu nkuoneshe walichokua wakimpa Chris kuvaa! ila suruali ya chupa kwa vijana ni fashion, mi tatizo ni kwenye viatu, nahisi angevaa mwanamke vinge nishawishi! au we unaonaje?



hebu ona walichomvalisha superstar huyu! pengine mi ni mshamba ama mshamba , ndo maana nastaajabu haya ya Brizzy ntajaona mengine ntaachama kinywa we acha tu! sasa hii ni jumpsuit ya mwanaume? au? nauliza kwasababu mi kwenye style na fashion baaado sana!



huu ni unyayo wake! upo hapo?alitupiamo kiatu kingine cha disgner ambaye sijapata jina lake bado!



huyu ndo alochukua nafasi ya Rihanna a.k.a Riri, bibi huyu anaitwa Karrueche Tran ! ana kitu nyuma ya mguu akipendacho wacha nikupe hapo chini! hata Riri anacho! ila kila mmoja ana tatoo ya iana yake.



              tatoo ya Karueche zipu hiyo bibi ooops so sorry na mabwana pia!



                                                                 kwa upana wake! umeonaaa?




                                             mguu wa kimwana Rihanna!




                                                        hizi ni za Rihanna nyuma ya titi! na mkonowe




                              hizi ni kwa uchache kabla hajajaza mwili wake kwa tatoo
                                                                                

                                                          SIKU NJEMA!

Wednesday, August 29, 2012

Rais Zuma azua jambo Bondeni.!!


               Rais wa Africa kusini Jackob Zuma

Kamisheni inayojishughulisha na masuala ya usawa wa kijinsia nchini Africa Kusini walipokea malalamiko kutoka kwa chama cha  Democratic Alliance  kuhusiana na  rais Jacob Zuma kutokana na maneno ama nasaha alizozitoa dhidi ya wanawake akiwa katika mahojiano hai kwenye television ya SABC3  nchini humo.
Kamisheni hiyo inashughulikia malalamiko hayo na kutolea ufumbuzi.
Zuma alitoa maoni yake wakati wa mahojiano na  Dali Tambo katika show yenye jina la watu wa Africa Kusini,kipindi hicho kilirushwa siku ya jumapili na interview hiyo ilifanyika nyumbani kwa rais huyo huko  Inkandla.
Lakini pamoja na hayo yote ama pengine!  Sintofahamu hiyo imetokea wakati wa harusi ya bintiye kipenzi! Ndio, kwani Rais Zuma hivi karibuni alipata mkwe kutoka kwa bintiye kipenzi Duduzile  na mkwe huyo ni Lonwabo Sambudla,na hisia za raisi  Zuma alizieleza wazi kua anaona fahari juu ya bintiye kwa hatua aliyofikia.

                                             Duduzile Zuma
 Na sababu kuu ya furaha yake ni kwamba anadai kua hakupenda kukaa na binti amabaye hajaolewa! Kwasababu kua single katika jamii ni tatizo,ila anafifikiri  iko dhana miongoni mwa watu wanaodhani kua single ni kitu kizuri,kiukweli hali hiyo si nzuri asilani, na ni ajabu!

                                     Siku ya pete!

Anasema kwa mwanamke unapaswa kua na watoto! Watoto ni muhimu kwa mwanamke na si muhimu tu bali ni mafunzo ya ziada kwa mwanamke pindi azaapo na kua mama.
Chama hicho cha  Democratic Alliancekinautazama usemi wa rais  Zuma kama umekaa  kimahaba zaidi na una jambo ndaniye dhidi ya wanawake  .
Wimbo alochagua binti huyo katika harusi yake ni wa Shania Twain uitwao  from this moment on!
Shuhudia kidogo harusi hiyo kati ya Duduzile na Lonwabo Sambudla.


               baba na mwana, baba Zuma wakati anamuingiza kanisani Bintiye



                                  Maharusi Duduzile na bwana harusi Lonwabo



                                                                  Busu la Kwanza



          na busu hilo hapo juu shurti upitie hatua hii ya kuuza uhuru wako, ndipo utabusiwa!





                                                                        Meza kuu!



                                                            Jikeki lilikuwepo kukamilisha furaha yao!



                                     baada ya hapo furaha ilitawala!!!!



                            Rais Zuma hakusita kuonesha furaha yake kwa tukio hilo kubwa




                                                                 kifamilia zaidi!



                                          huu ndo unyayo wa siku ya harusi yake


kama walivyo wa Ghana na Nigeria , South Africa nao huwa na harusi ya kimila, maharusi hawa nao walipitia hatua hiyo na ndivyo wanavyoonekana!



                                       akiwa katika vazi la kitamaduni bi  harusi Duduzile


tusubiri kusikia hatma ya wanaharakati hao juu ya kauli ya Rais Jackob Zuma dhidi ya wanawake.

Tuesday, August 28, 2012

Mwana anga mkongwe wa Marekani afariki dunia



                                                       Neil Armstrong

Rais Obama ameongoza katika sifa na rambi-rambi zilizotolewa baada ya kifo cha Neil Armstrong, mwana anga wa kwanza kutua kwenye mwezi, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 82 kutokana na matatizo aliyopata baada ya upasuaji aliofanyiwa kwenye moyo.
Rais Obama alimuelezea Neil Armstrong kwamba ni mmoja kati ya mashujaa wakubwa wa Marekani, siyo wakati wake tu, lakini katika historia ya nchi hiyo pia.
Mwenzake Armstrong katika safari ya kihistoria ya kwenda mwezini mwaka wa 1969 alikuwa Buzz Aldrin, ambaye alisema Armstrong alikuwa rubani na kamanda mahiri.

                                                       Buzz Aldrin

Familia ya Neil Armstrong imetoa wito kwa Wamarekani kuonesha heshima zao kwa kufuata mfano wake wa kutumika, kufanikiwa na bila ya majivuno.
Taarifa ya familia iliwaambia wale washabiki wake: "ukitembea nje usiku ukaona mwezi unakuchekea, mfikirie Neil na umkonyeze."

Friday, August 24, 2012

Hii Si Kawaida, Ila Imetokea,Nepal


                               Mohammed Salmodin jasiri aliyeua cobra kwa meno


mkulima mmoja jasiri  aliyekua ameng’atwa na nyoka aina ya cobra hakukubali kirahisi kufa peke yake alichoamua ni kumvizia nyoka huyo aina ya cobra na yeye akamng’ata hadi kifo cha cobra huyo, ni ujasiri wa iana yake! ndio maana nikamwita mkulima jasiri.

                    cobra mwenyewe mwenye futi 6, mwenzangu unaweza?

mohammed salmodin alipofanya shughuli hiyo ya kuling’ata joka hilo, hakuliachia mpaka alipoanza kuhisi kua joka hilo limekufa baada ya kumdondokea maungoni  huko nepal .cobra huyo alikua na urefu wa futi 6  na mohammed aliamua kumng’ata ng’ata cobra huyo  hadi kumuua.
mkulima huyo kazi yake kubwa ni kilimo cha mpunga, na alipokutana na  waandishi wa habari alitoa ushuhuda wake kwamba aliwahi kuambiwa na mtaalamu wa masuala ya nyoka kwamba, nyoka akikung’ata, na wewe mng’ate usimuachie  hadi afe na hakuna kitakachokutokea wewe! ndicho alichofanya.
anaendelea kusimulia kua alipotanabahi kua ameng’atwa na nyoka, akarudi nyumbani na kutafuta tochi na alipomtafuta nyoka huyo akagundua nyoka aliyemng’ata ni aina ya cobra hivyo akajipa ujasiri na kumng’ata hadi kifo!
mohammed ambaye kwa asili  maumbile yake ni mwembamba hakufikiria kwenda hospitalini kabla hajamuua nyoka huyo kama alivyowahi kuambiwa  na hii ni  baada ya kutiwa moyo na jirani zake ambao walimtaka asimuachie hivi hivi nyoka huyo na aina ya  cobra.
inasadikika kua mkulima huyo aling’atwa na cobra wa kawaida wanaoishi katika kijiji aishicho kilichoko maili 125 kusini mashariki mwa mji wa kathmandu
na inakadiriwa kwamba watu wapatao elfu 20,000 huumwa na nyoka aina hiyo huko nepal kila mwaka na kusababisha vifo vya watu 1,000 kwa mwaka.

Mke wa Mtu ni Sumu, Kinyozi Yamkuta


hisia zake zimemponza Khan! yakamkuta

Polisi nchini Pakistan imesema kinyozi YOUSAF KHAN  anapata nafuu katika hospitali moja nchini Pakistan  baada ya kukatwa baadhi ya viungo mwilini  mwake kufuatia kuwa na mahusiano na Mwanamke aliyeolewa katika familia moja ya kifahari katika wilaya ya Okara.
YOUSAF KHAN, mwenye umri wa miaka 32, alitekwa nyara na wanachama  7 wa familia ya mwanamke huyo na kumdunga macho yake kwa kisu kabla ya kumkata masikio, pua, ulimi na mdomo wake.

baada ya adhabu

Tukio hilo lilitokea siku ya jumanne katika kijiji cha Mirzapur nchini Pakistan.

                                                   Eneo la tukio

Afisa mmoja wa polisi anayechunguza kisa hicho, KHALIQ RIAZ, amesema tayari wamewatia nguvuni watu watano.

Hata hivyo, familia ya msichana huyo imesema ilikuwa imetoa onyo kwa kijana YOUSAF kuachana na uhusiano huo, lakini hakusikia, na ndio maana wakaamua kuchukua hatua hiyo ili kumuadhibu kinyozi huyo. Uhusiano huo unasemekana ulidumu muda wa miaka miwili.
pamoja na hayo leo ni ijumaa naomba nikutakie ijumaa kareem.

Thursday, August 23, 2012

Mwili wa Zenawi Wasubiri Maziko


                            Melez Zenawi wakati wa uhai wake.

Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Melez Zenawi, uliwasili katika mji mkuu wa nchi ya Adis Ababa na umehifadhiwa katika Ikulu hadi mazishi yake yatakapofanyika.



                                   Mwili wa Zenawi ukiwasili

Maelfu ya raia wa nchi hiyo walimiminika katika barabara za mji huo wakati mwili wake ulipowasili kutoka mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.Meles, ambaye alikuwa na umri wa miaka 57, aliaga dunia ghafla kutokana na maambukizi wakati alipokuwa akitibiwa.


                                      baada ya mzio hali mbaya

Kifo cha Bwana Zenawi kimezua hofu ya kugombea madaraka hali ambayo ingeweza kuathiri amani ya nchi hiyo.Kwa mujibu wa vyombo vya habari, naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn ataliongoza taifa hilo hadi mwaka 2015 wakati uchaguzi mkuu utakapofanyika.

                           Hailemariam Desalegn Mrithi  wa Zenawi

Utawala wa Bwana Zenawi ulishutumiwa kwa kukandamiza upinzani na kuna hofu kuwa Waziri Mkuu mpya huenda asiwe na uzoevu wa kushughulikia na kutatua uhasama wa kisiasa unaoendelea nchini humo.
Zenawi amesifika kwa kuiongoza Ethiopia kufikia mafanikio makubwa ya maendeleo na uchumi, lakini wakosoaji wake wanasema licha ya hayo yote utawala wake haukuruhusu uhuru wa siasa za vyama vingi na kuwa viwango vya ukiukwaji wa haki za binadam bado viko juu.
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.Meles Zenawi aliingia madarakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.

Viatu Vyenye Kisigino zaidi ya Inchi 5 Ni hatari Ki afya

Viatu vyenye visigino virefu vinaweza kuwasababishia akina dada matatizo ya uzazi imebainika.

Dax Moy ambaye ni mtaalamu wa kuwafundisha walimbwende namna ya kupozi, anadai kwamba viatu hivyo hasa vile vinavyofikia inchi tano na zaidi, vinamlazimisha msichana kukaa katika pozi zisizo za kawaida ambazo husababisha matatizo ya uzazi pindi atakapo hitaji kua nao.

Licha ya akina dada wengi kutambua matatizo ya viatu virefu ya mgongo, enka na miguu, wengi wao hawajui kwamba viatu hivyo vinaleta madhara kwenye viungo vya ndani ya mwili hasa via vya uzazi.
Moja ya matatizo makubwa ni kwamba jinsi viatu vinavyozidi kuwa virefu, vinasababisha sehemu ya chini ya tumbo kuegemea mbele, ambayo huleta maumivu ya mgongo .

Sehemu ya chini ya tumbo ni kama chombo cha kuhifadhia viungo vya ndani ya mwili, kila kitu kinatengewa nafasi ya kufanyia kazi yake.

Sehemu hii ikibinuka kwa mbele, viungo vya ndani vinabaki vimepandiana na kukuacha ukijisikia kama una msongamano au mvutano kwenye maeneo hayo.
Msichana unapojisikia uzito kwenye sehemu za chini ya tumbo, mara nyingi ni kwa sababu viungo vya ndani ya mwili vinaegemea upande wa mbele ya tumbo.

 Na kwasababu hiyo basi! Hii inaweza kupunguza ufanisi ndani ya tumbo na kuleta matatizo ya hedhi ambayo hatimaye husababishia wasichana kushindwa kushika mimba  .

Mi nilishindwa zamani kuning’inia , na siweki hapa kuwavunja moyo! Lah hasha!  bali hii ni kwa taarifa yako tu! Enjoy your heels! Zitakazo kupa miondoko yenye kuvutia!  Naomba nikutakie asubuhi njema.

Wednesday, August 22, 2012

Chui akutana na Rafikiye wa Zamani Baada ya Miaka 13


                                                                              old friend eh!

Bwana  Alberto Lena ameungana tena na rafikiye chui mwenye jina ambalo siwezi kuliweka hapa kutokana na mila na desturi zetu kua ni tusi ama kiungo cha uzazi cha jinsi  ya ------- , amabye alikua  Shamwari Game Reserve huko Eastern Cape. Lena alimuokoa chui huyo kutoka kwa wawindaji haramu huko Ivory Coast  miaka 13  iliyopita.




Kawaida ni kama sheria! Unapokwenda kumtembelea mtu shurti ubebe zawadi! Jamaa alibeba zawadi kwa ajili ya rafikiye! akampa




bila shaka ni tamuuuuuu! au siyo? lakini je unamkumbuka mshkaji wako?mtazame tena basi!




baada ya kula akamtazamaaaaa! je unadhani anamkumbuka? sidhani




aaaagh vipi tena? urafiki umeisha mara? mbona zawadi ulikula?

kiukweli napenda sana wanyama! lakini urafiki na mnyama kama Simba,Chui, Tembo na wengineo mh hapana! wazuri kuwatazama kwa mbali na kutukuza uumbaji ila kwa karibu? labda awe kafa! sorry. kiukweli anaweza kukubadilikia anya time hapo tu mi ndo imani hua inantoka! HAWAFUGIKI!