Thursday, August 23, 2012

Viatu Vyenye Kisigino zaidi ya Inchi 5 Ni hatari Ki afya

Viatu vyenye visigino virefu vinaweza kuwasababishia akina dada matatizo ya uzazi imebainika.

Dax Moy ambaye ni mtaalamu wa kuwafundisha walimbwende namna ya kupozi, anadai kwamba viatu hivyo hasa vile vinavyofikia inchi tano na zaidi, vinamlazimisha msichana kukaa katika pozi zisizo za kawaida ambazo husababisha matatizo ya uzazi pindi atakapo hitaji kua nao.

Licha ya akina dada wengi kutambua matatizo ya viatu virefu ya mgongo, enka na miguu, wengi wao hawajui kwamba viatu hivyo vinaleta madhara kwenye viungo vya ndani ya mwili hasa via vya uzazi.
Moja ya matatizo makubwa ni kwamba jinsi viatu vinavyozidi kuwa virefu, vinasababisha sehemu ya chini ya tumbo kuegemea mbele, ambayo huleta maumivu ya mgongo .

Sehemu ya chini ya tumbo ni kama chombo cha kuhifadhia viungo vya ndani ya mwili, kila kitu kinatengewa nafasi ya kufanyia kazi yake.

Sehemu hii ikibinuka kwa mbele, viungo vya ndani vinabaki vimepandiana na kukuacha ukijisikia kama una msongamano au mvutano kwenye maeneo hayo.
Msichana unapojisikia uzito kwenye sehemu za chini ya tumbo, mara nyingi ni kwa sababu viungo vya ndani ya mwili vinaegemea upande wa mbele ya tumbo.

 Na kwasababu hiyo basi! Hii inaweza kupunguza ufanisi ndani ya tumbo na kuleta matatizo ya hedhi ambayo hatimaye husababishia wasichana kushindwa kushika mimba  .

Mi nilishindwa zamani kuning’inia , na siweki hapa kuwavunja moyo! Lah hasha!  bali hii ni kwa taarifa yako tu! Enjoy your heels! Zitakazo kupa miondoko yenye kuvutia!  Naomba nikutakie asubuhi njema.

No comments:

Post a Comment