Mohammed Salmodin jasiri aliyeua cobra kwa meno
mkulima mmoja jasiri aliyekua ameng’atwa na nyoka aina ya cobra hakukubali kirahisi kufa peke yake alichoamua ni kumvizia nyoka huyo aina ya cobra na yeye akamng’ata hadi kifo cha cobra huyo, ni ujasiri wa iana yake! ndio maana nikamwita mkulima jasiri.
mohammed salmodin alipofanya shughuli hiyo ya kuling’ata joka hilo, hakuliachia mpaka alipoanza kuhisi kua joka hilo limekufa baada ya kumdondokea maungoni huko nepal .cobra huyo alikua na urefu wa futi 6 na mohammed aliamua kumng’ata ng’ata cobra huyo hadi kumuua.
mkulima huyo kazi yake kubwa ni kilimo cha mpunga, na alipokutana na waandishi wa habari alitoa ushuhuda wake kwamba aliwahi kuambiwa na mtaalamu wa masuala ya nyoka kwamba, nyoka akikung’ata, na wewe mng’ate usimuachie hadi afe na hakuna kitakachokutokea wewe! ndicho alichofanya.
anaendelea kusimulia kua alipotanabahi kua ameng’atwa na nyoka, akarudi nyumbani na kutafuta tochi na alipomtafuta nyoka huyo akagundua nyoka aliyemng’ata ni aina ya cobra hivyo akajipa ujasiri na kumng’ata hadi kifo!
mohammed ambaye kwa asili maumbile yake ni mwembamba hakufikiria kwenda hospitalini kabla hajamuua nyoka huyo kama alivyowahi kuambiwa na hii ni baada ya kutiwa moyo na jirani zake ambao walimtaka asimuachie hivi hivi nyoka huyo na aina ya cobra.
inasadikika kua mkulima huyo aling’atwa na cobra wa kawaida wanaoishi katika kijiji aishicho kilichoko maili 125 kusini mashariki mwa mji wa kathmandu
na inakadiriwa kwamba watu wapatao elfu 20,000 huumwa na nyoka aina hiyo huko nepal kila mwaka na kusababisha vifo vya watu 1,000 kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment