hisia zake zimemponza Khan! yakamkuta
Polisi nchini Pakistan imesema kinyozi YOUSAF KHAN anapata nafuu katika hospitali moja nchini Pakistan baada ya kukatwa baadhi ya viungo mwilini mwake kufuatia kuwa na mahusiano na Mwanamke aliyeolewa katika familia moja ya kifahari katika wilaya ya Okara.
YOUSAF KHAN, mwenye umri wa miaka 32, alitekwa nyara na wanachama 7 wa familia ya mwanamke huyo na kumdunga macho yake kwa kisu kabla ya kumkata masikio, pua, ulimi na mdomo wake.
baada ya adhabu
Tukio hilo lilitokea siku ya jumanne katika kijiji cha Mirzapur nchini Pakistan.
Afisa mmoja wa polisi anayechunguza kisa hicho, KHALIQ RIAZ, amesema tayari wamewatia nguvuni watu watano.
Hata hivyo, familia ya msichana huyo imesema ilikuwa imetoa onyo kwa kijana YOUSAF kuachana na uhusiano huo, lakini hakusikia, na ndio maana wakaamua kuchukua hatua hiyo ili kumuadhibu kinyozi huyo. Uhusiano huo unasemekana ulidumu muda wa miaka miwili.
pamoja na hayo leo ni ijumaa naomba nikutakie ijumaa kareem.
No comments:
Post a Comment