Friday, August 17, 2012

Koffi Amdunda Produser wake?!


                        KOFFI OLOMIDE

Mwanamuziki mashuhuri barani Afrika, KOFFI OLOMIDE ameshitakiwa kwa kumpiga Mtayarishaji wake wa muziki makofi na kuumizi mdomoni.
Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani siku ya jumatano kutokana na kuhusishwa na vurugu zilizotokea katika hoteli moja mjini Kinshasa na wakati wa vurugu hiyo inasemekana Koffi aliharibu baadhi ya mali za hoteli hiyo ukiwemo mlango wa hoteli hiyo na mali kadhaa za Lubaki ziliharibiwa.



Watu wengi walijitokeza katika Mahakama hiyo ya Kinishasa kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo imeharishwa hadi Alhamisi asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.Wakati wa kesi hiyo KOFFI OLOMIDE aliwakilishwa na mawakili 10.
Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake wa album ya Adakadabra  Bwana  DIEGO LUBAKI, ni kuhusu pesa dola $3,680


                                                     Diego Lubaki


Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi sita.
Mmoja wa mawakili wa waliokuwa wakimtetea Mwanamuziki huyo LWEMBA MUYABO amesema walikuwa wanaamini kuwa mteja wao ataachiwa kwasababu promota alikubali kuondoa kesi hiyo.

Mashuhuda watatu wote waajiriwa wa  hoteli hiyo ya Venus,walitoa ushahidi wao kwa alichokifanya Koffi kwa alichomfanyia Lubaki

Wawili kati ya hao walisema kua walimwona kiongozi wa bendi hiyo ya orchestra Latin Quarter akimpiga Diego Lubaki, wakati wakigombea suitcase ambayo inadaiwa kua ni mali ya Lubaki .
Shahidi watatu ambaye ni menejwa hoteli hiyo ambaye ni mwana mama alisema kua alimwona Koffi akiingia katika chumba ambacho  Diego Lubaki alikua akikaa bila watu wa mapokezi kutaarifiwa  
Wawili wa mwanzo walisema kua walimwona Koffi akiwa amebeba   elevator kuelekea kwenye chumba cha Diego.
Hata hivyo kutokana na mchanganyo huo wa mambo upande wa utetezi ulijinasibu kua hakuna ushahidi wa dhiri na kudai kua mteja wao hana hatia.

Chumba cha Mahakama kilifurika wasanii kibao,waandishi habari ambao Koffi huko nyuma pia aliwahi kumpiga walau mmoja na washabiki wa Koffii pia walikuwepo , na wawili kati yao walitiwa ndani kwa makelele ya kumtetea Koffii kua hana hatia.

Antoine Akgepa, Alias Koffi Olomide mwenye mchanganyo wa congo-Sierra Leoneaalizaliwa  August 13, 1956 huko  Zaire ya zamani leo hii ni jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Koffi ndoto zake ilikua aje kua mcheza mpira mahiri duniani lakini alipokua motto alianza kuvutiwa na muziki taratibu! Akiwa mapumzikoni mnamo mwaka 1978 mjini  Kinshasa alirejea likizo kutoka Ufaransa alikokua akisoma na akarekodi wimbo wake wa kwanza mnamo mwaka 1983 ndio mwaka wa safari yake ya kimuziki ilipoanza rasmi kwa album ya Ngounda.
Baada ya miaka 3 akaunda kundi maarufu hii leo la Latin Quarter ambalo kiongozi alikua yeye na kuzinduliwa kwa kundi hilo kulifanya auze album yake ya Noblesse obliges.

mwaka 1994,alipewa tuzo ya  Meilleur na  Africa Music Awards  na kufanikiwa kuliteka soko la kimataifa na kumletea mafanikio makubwa. Na hilo lilimletea tuzo nne za  Kora mnamo mwaka  2001 na tuzo ya  msanii bora wa karne mwaka  2005 katika tuzo za kora  Koffi ni msanii na mwanamuziki mwenye album lukuki katika soko katika Jamhuri yote ya Kidemokrasia ya Congo, hii ndo kazi ya Diego, tazama upishi wake katika Abra Kadabra. twendeeeee

No comments:

Post a Comment