Hawa Ngulume enzi za uhai wake.
Bi Hawa Ngulume, aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Bagamoyo na Mbarali, amefariki dunia jijini Dar es Salaam. Mama Ngulume amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa kwa kipindi kirefu na mauti yamemfika akiwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar.
Kwa kujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana taratibu za mazishi na maziko zinaandaliwa na taarifa kamili itatolewa.
Mungu ailaze roho ya marehemu HAWA NGULUME mahali pema peponi. AMINA
No comments:
Post a Comment