Monday, September 3, 2012

Watoto na Maajabu yao!


                                                          tulieni! hana noma huyu.

Hali ya utoto ni raha sana , kichwa kinakua kitupu na huna mawazo yoyote! Hata kujieleza uwapo na shida si rahisi, kikubwa utalia na mtu pekee aliyepewa uwezo wa kung’amua shida zako ni mama yako mzazi! Asante mama. Ni upeo na uwezo wa kipekee mno, na hata motto anapojifunza kuzungumza ni mama yake tu ndiye ambaye huwa an uwezo wa kufumbua motto ana maanisha nini!
Mtoto pia ,Mungu alimpa uwezo mkubwa sana kuona yasiyoonekana na wakipata kitisho huwa wanalia ama kukumbwa na homa kali. Lakini Mungu aliwaficha wenye hekima na akili yale alowafunulia watoto!
Watoto pia wana vutia kuwatazama ama kuongea nao, watoto pia wawapo kwenye familia huwa ni furaha na wanapokosekana huwa ni huzuni ya ajabu mno!watu husimangwa na ndugu wa mume kwa kukosekana motto katika familia bila kuchunguza pengine lipo tatizo la kuwasaidia wanandoa kulitatua kwa amani bila kuwasumbua kwa maneno,.
Mtoto  pia hua anapewa nafasi ya kipekee  na ulinzi hata na wanyama wakali, ama hata wenye sumu ya kuwaua! Wao huweza kuwaacha wawatambae, ama kuwazinga ama kutia hata mkono kinywani mwa simba mfalme wa pori nab ado motto asidhurike! Kinachotufanya sisi watu wazima kupata madhara kutoka kwa wanyama ni ile hali ya taharuki tuipatayo pindi tuwaonapo wanyama wakali ,wakutisha ama wenye sumu kali! Mwili hapo hua unatoa harufu ambayo mnyama kwa majaaliwa yake hupata ujumbe kua mtu aliyeko mbele yake anajiandaa kwa shari, basin a wao hujipanga na kutushambulia!

Kinachonifanya nisema ni huyu dogo!  Hapa chini


Mi ningezimia siku nyingi badala ya kutabasamu kama dogo huyu afanyacho!!!!

anacheza naye kama yuko na mtoto mwenzie! jaribu wewe mtu mzima uone cha moto! acha watoto wapewe baraka zao.Charlie Parker anataka atambulike kama mtunza wanyama mdogo anayeinukia. upo hapo?

                  mhhhh haya weee!! Charlie mi sikuwezi!babake Charlie aitwae Greg anamiliki  zoo ya wanyama ya Ballarat huko Victoria South Africa, mtoto huyo ambaye hana woga hata kidogo alikua akicheza na nyoka huyo mwenye kilo kumi , dogo ana kama miaka 2 hivi tayari ni mtaalamu wa wanyama watambaao! name them.

                  uuuuh je unayaweza? dogo kweli mkali!


                       huyu mamba huyu siyo? aaaagh eh

         kilo kumi sio kidogo kwa Charlie , si unaona ana feel uzito!

        dogo Charlie ana shughuli na dubwana hilo! ah mi basi bana!

Nilipoona picha yake asubuhi ya leo! Nilichanganyikiwa! Kwasababu mnyama huyo aliyembeba hata apite mbali name kiasi gani mi siko tayari hata kumuona! Namuogopa sana kiukweli! Mh Fiesta ya mwaka wa jana pale Manzese nililishuhudia moja lililoletwa pale kwa michezo nilihamanika sana baada ya kupewa taarifa kua ataletwa uwanjani hapo kua sehemu ya burudani! I was whaaaaaat? Burudani? Mmekosa kweli cha kuleta mpaka mumlete huyo mdudu hapa? Haikubadilisha kitu! Aliletwa na nilikamatwa nikapelekwa kwa karibu, nlichoomba tu ni kwamba sitaki kuona kichwa chake.
Kweli   kichwa  kikikwepeshwa nikamtazama kwa fadhaa basi nikajitia ujuaji nikamgusa gusa! Weeeee ana magamba kwenye ngozi yake hatari na kila navyo kupitia ana nata na wewe! Utajuta! Mi mmmmmmh hapa KWELI MUNGU KAUMBA NA ANASTAHILI SIFA,UTUKUFU NA SHUKRANI ! MAANA ANATISHA KWA UBUNIFU NA UUMBAJI WA KIPEKEE NA  HAKUNA KAMA MUNGU BABA WA MBINGUNI!

No comments:

Post a Comment