KARDINAL LAURIAN RUGAMBWA 1912----1997
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwaongoza wakaazi wa mkoa wa KAGERA katika kumbukumbu ya kumuenzi aliyekua Askofu mkuu wa Kwanza wa kanisa Katoliki Tanzania Mwadhama KARDINAL LAURIAN RUGAMBWA inayotarajiwa kufanyika oktoba sita mwaka huu mkoani humo.
Askofu mkuu msaidizi jimbo la Bukoba METHODIUS KILAINI
Akizungumza jijini Dar-Es –Salaam, Askofu mkuu msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Bukoba, METHODIUS KILAINI amesema kwamba katika hafla hiyo shughuli mbalimbali zinatarajiwa ikiwemo ile ya kuhamisha mabaki ya mwili wa Hayati KARDINAL LAURIAN RUGAMBWA na kuhifadhiwa katika sehemu maalum kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
KARDINAL LAURIAN RUGAMBWA kulala upya humu
July 12 mwaka huu alitimiza miaka 100 na october 6 mwaka huu atazikwa upya na hii ni kumbukumbu kuu si kwa Bukoba tu bali Tanzania na nchi jirani so kufanikisha hayo yote mawili kufanikiwa kifedha Askofu msaidizi ana ombi! Msije sema ni maneno yangu soma mwenyewe! To assist with financial costs, logistical planning, material, volunteer, email: Rt. Rev. Bishop Method Kilaini: mkilaini@gmail.com & Fr. Adeodatus Rwehumbiza: arweyhufr@yahoo.it
No comments:
Post a Comment