Uamuzi wa
Muungano huo umefikiwa kufuatia ripoti ya baraza la usalama la Umoja huo
iliyodai kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23 dhidi ya serikali ya Congo.
Waasi hao
wanadhibiti kimabavu sehemu kubwa ya Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo na hata kuwatoza kodi wananchi.Kundi hilo lilianza uasi katika eneo hilo
mwezi Aprili na kusababisha takriban watu nusu milioni kukimbilia usalama wao.
Umoja wa
Mataifa unafanya mkutano na baadhi ya yatakayopewa kipaombele kwenye mkutano
huo ni swala la mgogoro huo Mashariki mwa Congo.Mapema mwezi Julai Marekani
ilizuia dola 200,000 zilizokusudiwa kulisaidia jeshi la Rwanda.
Msaada
wenyewe uliokatwa siyo mkubwa kwa jeshi la Rwanda, lakini hatua hiyo ilitoa
ishara kubwa.Kwa kukata msaada huo, Marekani ni kama ilikuwa inasema
"tunaamini ripoti kuwa Rwanda inatibua usalama wa kanda hiyo kwa kuwaunga
mkono wapiganaji wa Congo".
Mwezi Juni
,Umoja wa Mataifa ulikabidhi ripoti kwa Baraza la Usalama, ambayo ilisema ina
ushahidi mzito kuwa Rwanda inalipatia kundi la M23, wapiganaji na zana, na
kurahisisha makamanda wao wakubwa kusafiri na kuvuka mpaka baina ya Congo na
Rwanda.Uasi huo ulianza mwezi wa Aprili, wakati wanajeshi mia kadha wa jeshi la
Congo walipofanya ghasia.
Wanawake
Mashariki mwa Congo wakilaani maasi
Uasi huo
uliongozwa na Jenerali Bosco Ntaganda, ambaye anasakwa na Mahakama ya Jinai ya
Kimataifa, ICC, kwa uhalifu wa kivita.Nayo serikali ya Uholanzi ilisitisha
msaada wa dola milioni 6.15 kwa Rwanda baada ya nchi hiyo kuhusishwa na madai
hayo ingawa baadaye ilianza tena kutoa msaada kwa nchi hiyo baada ya serikali
ya Rwanda kuahidi kushirikiana na kukomesha vita hivyo.
No comments:
Post a Comment