Wednesday, September 26, 2012

KATY PERRY NDIYE BILLBOARDS WOMAN OF THE YEAR

Cast member and singer Katy Perry poses during a photocall before the premiere of ''Katy Perry: Part of Me'' in Rio de Janeiro July 30, 2012. REUTERS/Ricardo Moraes


Pop star Katy Perry  ametajwa jana kwamba ndiye mwanamke aliyefanya vizuri sana katika chati za Billboard's  na atapewa tuzo ya Billboard's Woman of the Year, nah ii ni baada ya kung’ang’ana kwenye chati hizo kwa miezi 12  na huo ndio wakati amabao alikua ametalikiana na mumewe na alihit katika single na filamu  .
Perry, mwenye umri wa miaka  27, alitalikiana na mumewe mwenye asili ya Uingereza mchekeshaji   Russell Brand  mwishoni mwa mwaka wa jana na wakati huo single yake ya "Part Of Me" ilikua juu ya chart hizo na   filamu ya 3D  ya behind-the-scenes ikimuonesha "Katy Perry: Part Of Me"  ambayo inayahusu maisha yake kitaaluma kupanda na kushuka ikiwa ni pamoja na mahusiano yake.
Ushindi wake umeanzia kwenye ukurasa wa mashabiki wake katika kurasa za Twitter na Facebook  ujulikanao kama katycats na vilivyompa umaarufu ni  costumes zake na  bubble gum pop songs.
Jarida la Forbes  limempaisha Perry katika nafasi ya 3  kati ya wanawake wanamuziki wenye mkwanja mrefu mpaka kufikia December 2011, inakadiriwa kua alikua ana mkwanja wa dola milioni 44.


Mpaka sasa amesha uza kazi zake milioni 48 katika nchin ya  Marekani pekee nah ii ni kwa muujibu wa , Billboard,hii inajumuisha hit zake kali kama  "Firework," "California Gurls," "E.T." na  "Hot N Cold" kutoka katika  label  yake ya mwaka 2008 "One Of The Boys"  na  albam ya  mwaka 2010 iitwayo  "Teenage Dream."
Perry hujipamba mno na hasa kucha zake na macho yake na huitunza mno ngozi yake japokua anapenda vitafunwa Popchips.
Kwa muujibu wa jopo la Billboard's la madirector  wakiongozwa na Bill Werde  wameeleza vigezo vyao kua Perry alichaguliwa kwa mafanikio yake na kumbatiza kua "one of the most exciting and inspiring artists in the industry."
Perry hayuko peke yake bali wamo pia  Taylor Swift, Beyonce na na  mwanamuziki kutoka kundi la Black Eyed Peas mwimbaji  Fergie.
Perry atapokea tuzo yake katika sherehe za  Billboard Women in Music mwaka huu mjini  New York  mnamo November 30.


No comments:

Post a Comment