Rais wa zamani wa Zambia, Kenneth
Kaunda
Rais wa
zamani wa Zambia Kenneth Kaunda jumamosi
iliyopita alilazwa hospitalini katika hospitali ya University Teaching Hospital
kutokana na ugonjwa uso julikana ama
pengine niseme kihoro na kusababisha ibada ya maziko ya mkewe iahirishwe! Na huo
ni uamuzi wa familia yake,
Mke wa Rais
huyo wa Zamani wa Zambia bibi Betty alifariki jumatano ya wiki ilokwisha akiwa
na umri wa miaka 83 akiwa nchini Zimbabwe ambako alikwenda kumtembelea binti
yake. Na maafisa wa serikali wanaeleza chanzo cha kifo chake kwamba alifia
usingizini nyumbani kwa binntiye aitwae Musata Kaunda-Banda katika jiji la Harare eneo la Borrowdale
Brooke.
Marehemu Bi Betty
Kaunda
Kufuatia kifo
hicho, serikali ya Zambia imetangaza siku 3 za maombolezo ya kitaifa na maziko
yake yatakua ya kiserikali na kwamba yangefanyika jana.
Kaunda mwenyewe alishiriki katika maandalizi ya
mazishi yalofanyika mjini Harare kabla ya mwili huo haijasafirishwa kwa ndege
kwenda Zambia, ukisindikizwa na maofisa kadhaa wa chama cha Zanu PF akiwemo mwenyekiti wa chama hicho Simon Khaya
Moyo, msemaji wa ZANU PF Rugare Gumbo, na wanachama wafuatao Nicholas Goche, Kumbirai Kangai, Oppah Muchinguri
na Victoria Chitepo.
Jeneza lenye
mwili wa Bi Betty Kaunda
Hizi ni
salamu za rais wa Africa Kusini Jacob
Zuma anamuelezea Betty Kaundakwamba
alishiriki kikamilifu wakati wa utafutaji uhuru wa Africa Kusini wakati wa
ubaguzi wa rangi.
Na ujumbe
wake kufuatia kifo hicho anaeleza kua , Betty alikua mpigania haki za wanawake
wakati wa ukoloni barani Africa,mchango wake utathaminiwa daima.
Enzi
hizo Kenneth Kaunda na bi Betty Kaunda, pole Mzee Kaunda! ile Lesso nyeupe naamini bado imo mikononi mwako itakusaidia kuyafuta machozi yako.
No comments:
Post a Comment