Michelle Obama
Mkewe Rais wa Marekani, Barack Obama, Michelle, amehutubia kongamano la chama tawala cha Democratic ambapo alitetea haki ya mumewe kupewa nafasi kutawala taifa hilo kwa muhula wa pili.
Akiongea Kaskazini mwa Jimbo la Carolina, alimtaja mumewe kama mtu anayeelewa matatizo yanayowakumba wamarekani.
Mama akiingia mkutanoni
Salaam! mi utege na fitness yake tu! ingawa najua kui zingatia si mchezo, mazoezi!
Michelle Alitetea hatua ya mumewe ya kuanzisha mpango maalumu wa bima ya afya ulioleta utata mwingi sana hasa miongoni mwa wanachama wa chama cha upinzani cha Republican walioupinga.
Alisema kuwa mumewe alinuia kutoa nafasi sawa ya matibabu kwa wote. Hata hivyo alikiri kuwa mageuzi aliyoahidi mumewe miaka minne iliyopita yalikuwa magumu kuyatekeleza lakini akasisitiza kuwa yatafaulu baadaye.
Rais Obama atahutubia kongamano hilo baadaye juma hili, ambapo atakubali rasmi kuwa mgombea wa Urais wa chama cha Democratic.
Muonekano huu mpya wa nywele za Michelle umepongezwa na wengi .
Kuomba kura muhimu, tena ki style, japokua alikua anatuma ujumbe kua kucha na nguo yake vinaendana! mama ya style aminiaaaa
Tukio lilikua live!
baada ya hotuba aliusogelea umati wa watu na kuwapungia! kampeni ilipendeza
kabla ya shughuli, ni maandalizi na ukaguzi! alikwenda kukagua jukwaa ambalo alilitumia
baada ya ukaguzi alimpa gwara, jamaa alosimamia maandalizi! kula gwara!
Rais Barak Obama anatarajiwa kuhutubia kongamano hilo leo. Ambapo atakubali rasmi kua mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Democratic
No comments:
Post a Comment