Mungu anaumba kiukweli! Na uumbaji wake haudanyi, na leo naomba nikuoneshe uumbaji wa Mungu ambao hauna subra katika vilivyoundwa na wana adam pindi wanapoingilia, ama kuweka mbele,karibu na miti hiyo yenye hasira , kwani hakuna pengine pa kuweka mpaka kwenye miti? Kuizunguushia vitu inahusu nini? Na yenyewe inataka kujiachia!
Miti haina midomo, hutoa sauti na harufu nzuri za manukato yake ya asili pindi upepo unapovuma ama kupuliza taratibu!
Miti imekua ikila alama za barabarani! Mawe ya makaburi, vibao vya chuma, huvimeza taratibu! Hadi vyote viishie ndani ya jimti hili! Leo wacha nikuoneshe nguvu na uweza wa Mungu iliyomo ndani ya miti! Pengine Mungu anasema nasi kupitia miti hiyo! Sijui najaribu kufikiri kwa njia ya picha!
Mbele ya mti kulikua na mlingoti wenye kibao hicho, leo hii mlingoti hauonekani na kibao ndo hichoooo kinaishia na ujumbe ulokusudiwa , itakua ni kudhani kama ni mgeni katika mji huo!
Kwa nchi za wenzetu wao huwa wanaweka urembo wa kuuzunguuka mti! Miaka inavyosonga mti hutanuka na kuonesha uwezo wake na kula taratibu kirembesho hicho! Hapa bongo huwa tunatupia tairi kwenye mti uliooteshwa ili kuzuia wanyama na watu waharibifu wasiufikie kwa karibu, Bagamoyo pale kuna mbuyu ambao una mnyororo ulioliwa na kubaki kipande cha mnyororo alofungiwa punda aliyewekwa pale! Niishie hapo maana pana historia ya kutiririka nayo!
Hili ni angalisho ambalo huwezi kupata ujumbe namna ulivyo ishia! Mwanzo unaweza soma chini sasa! Miti kulakula ama niseme yenye hasira na kazi ya mikono ya wanadamu!
Makaburini nako! Bila huruma miti mikubwa na minene ya miaka mingi humeza mawe yenye majina ya marehemu! Na hayo ni makaburi yaliyoko kwenye misitu mikubwa yaliyo katika maeneo tengefu, lakini kwa makaburi yaliyo kwenye mpangilio mzuri kidogo ahueni mawe, ama misalaba hailiwi!
Ukipita pwani ya Ocean road karibu na mamlaka ya chakula na dawa ama kwingineko utaiona miti mikubwa namna ilivyokula kingo za bahari ama hata kutifua kingo hizo kwa mizizi yake yenye nguvu! Moja ya miti yenye mizizi yenye hasira na nyumba za watu ni mwarobaini kiasi cha serikali pamoja na watu wa mazingira kukuzuia kuipanda karibu na nyumba! Kadhia yake sio ndogo! Tazama huu ulivyokula kingo .
Kibao hiki kilicholiwa, kinaonesha onyo la kuzuia mtu hapaswi kuingia katika msitu ulio nyuma ya mti huo, sasa umeliwa! Kwa mgeni unafanyaje utaelewa nini? Ama utaingia tu na yatakayo kukuta utayajua mbele ya safari? Hatari kwa mother nature kula kazi ya mikono ya wanadamu iliyoingilia himaya yake.
Hapa unafanyaje ikiwa ujumbe ulokusudiwa ukufikie umeliwa na mti wenye hasira?
Watch out for what sasa? Mti weee mbona huna huruma?
In short inawezekana miti haitaki kuingiliwa katika himaya zao! Na tusiweke vifaa vya vyuma karibu yake vinaliwa na ujumbe uliokusudiwa haifiki kwa walengwa waliokusudiwa! Siku njema mdau! Asante sana kwa kuitembelea KEGAJOBLOGSPOT.COM. asante sana!!!!!
No comments:
Post a Comment