Ni raha tele! bwana na bibi Tchangirai
WAziri mkuu
wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amefanikiwa kufunga ndoa yake siku ya Jumamosi
licha ya mahakama ya nchini mwake kumzuia kufanya hivyo!
Na hii ni
baada ya mke wa kimila kupeleka mashtaka mahakamani na kudai kwamba wao bado ni
mke na mume halali, kwa mila na desturi za kabila lao na sheria za kabila
hilo.mahakama hiyo ilielezwa kwamba waziri mkuu huyo Morgan Tsvangirai alilipa
mahari juu ya mwanamke huyo mwaka wa jana na kumuoa!
Waziri Tsvangirai mkewe mpya
Tsvangirai,mwenye
umri wa miaka 60, na bi harusi mpya Elizabeth Macheka,ambaye ana
miaka 35, walikula kiapo cha kua mke na
mume ingawa hawakusaini vyeti vya ndoa. Tsvangirai alisistiza kua hafanyi
makosa ya kuhukumiwa ama kua judged kwa kua na mwanamke mwingine na hii ni
tangu mke wake wa kwanza Susan aliyeishi
naye kwa takriban miaka 31 afe ajalini akiwa na umri wa miaka 50, mnamo mwaka 2009.utetezi huooo!
Bi harusi
alifanya kitchen party au pre wedding
Tsvangirai alijinasibu
kua walau sasa amempata mwandani sahihi. Na haikua kazi rahisi kwani ilimlazimu
kukutana na wanawake kadhaa ili kumpata mwanamke ampendaye na kuwashushua
waandishi wa magazeti waliozusha propaganda ambazo zimemfanya maisha yake binafsi
yawe hayana raha na kumshushia hadhi yake.
kama ada bi harusi shurti apeleke keki kwa wazazi na wakwe
Mwanamuziki mashuhuri
na nguli barani Africa na ulaya superstar Oliver Mtukudzi alikua kivutio katika harusi hiyo ya waziri
mkuu was Morgan Tsvangirai na mkewe mpya bi Elizabeth Macheka na aliwaimbia wimbo maalum uitwao ‘Svovi’ for
the ‘Premier’ walipoufungua muziki na kua special dance!.
maharusi wakiucheza wimbo huo wa ‘Svovi’ for
the ‘Premier’
hawa ni madj wa itifaki za kiserikali, walioachia burudani harusini nao ni DJ’s Kudzi Marudza, Witness Matema and Tendai Chakanyuka
No comments:
Post a Comment