Monday, September 3, 2012

R.I.P Daudi Mwangosi


                                                Marehemu Daudi Mwangosi enzi za uhai wake.

Mroki ni mwandishi wa habari na mmiliki wa mrokim.blogspot.com ameripoti kwamba mwandishi wa habari na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Daudi Mwangosi amefariki dunia kwenye kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa baada ya kutokea vurugu kati ya polisi na wafuasi wa chama cha Chadema.
Mwangosi ambae ni mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Channel ten, amefariki papo hapo ambapo vurugu zilitokea katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa september 2/ 2012  saa kumi jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa kwa risasi .
Kabla ya kifo chake, mabomu yalipigwa eneo hilo ili kuwatawanya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika.
Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kwake  kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo alitaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kipigo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo ambapo mwandishi huyo pamoja na askari mmoja wakaanguka chini .
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti ya askari huyo ikisema afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe na mabomu, zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa akiwemo mwanahabari mmoja Godfrey Mushi.

No comments:

Post a Comment