Klabu ya
waandishi wa habari mkoani Iringa –IPC nchini Tanzania, kwa kushirikiana
na waandishi wote wanaofanya kazi mkoani humo, kuanzia Jumanne
imetangaza kusitisha ushirikiano wa kikazi baina yao na jeshi la polisi mpaka
pale taarifa au majibu sahihi kutoka vyombo huru zitakapotolewa kujua
aliyemuuwa mwandishi wenzao Daudi Mwangosi wakati wa vurugu za chama cha
demokrasia na maendeleo -Chadema na polisi.
Kazi hizo ni pamoja na kuwataarifu waandishi wote kuacha kwenda katika ofisi ya kamanda wa polisi kupata taarifa za matukio mbalimbali .
Mwangosi ambaye pia ni mwandishi wa habari wa Chanel Ten alifariki Jumatatu majira ya saa 10 jioni baada ya kupigwa na kile kinachosadikiwa kuwa bomu katika vurugu za wafuasi wa Chadema waliokuwa wakitawanywa na polisi.
Kumezuka utata wa nani anahusika na tukio hilo huku jeshi la polisi likitoa taarifa jumanne kusema uchunguzi wake unaonesha kuwa bomu lililompiga mwandishi Mwangosi lilitoka upande wa Chadema.
No comments:
Post a Comment