Thursday, September 13, 2012

Sad News:Nonini na One FM wajitolea kumsaidia bondia wa kike aliyewehuka





Bondia bingwa mwanamke wa Kenya Conjesta Achieng tarehe 24 mwezi Desemba alimshinda mchezaji kijana wa Argentina Guillermina Fernandez bila kutumia nguvu nyingi na kupata ubingwa wa ngazi ya uzito wa katikati kwa wanawake wa shirikisho la ndondi duniani IBF baada ya kupata mkanda wa dhahabuwa baraza la ndondi la kimataifa WBC.




Katika mchuano huo wa kumtafuta bondia bingwa mwanamke, nguvu bora ya Conjesta Achieng ilionekana dhahiri, dakika 1 na sekunde 40 baada ya kuanza kwa pambano hilo, alifanikiwa kumweka Guillermina Fernandez kwenye kona kwa mashambulizi makali na kumlazimisha kocha wa Fernandez apeperushe taulo na kuonesha kushindwa.
Ushindi wake dhidi ya Fernandez umefanya jumla ya mafanikio ya Achieng yawe kushinda mara 21 na kushindwa mara 3. Mchezo huo ulifanyika katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Kenya ambao ulichelewa kufanyika kwa saa tano na kusababisha malalamiko kutoka kwa watazamaji. 

 





Conjesta alipewa jina la utani la ‘hands of stone’ kwa uwezo wake wa juu kwenye ndondi. Ni mkenya aitwaye  Conjestina Achieng’. Habari mbaya ni kuwa boxer huyu wa kwanza wa Afrika kuwahi kushinda taji la dunia amekuwa chizi.

Uchizi wake huu umetokana na kuvuta bangi na ulevi wa kupindukia. Kwa sasa anaishi na dada yake kwenye chumba ambacho ameshindwa kukilipia kodi kwa miezi minne.

Rapper wa Kenya Nonini akishirikiana na kituo cha radio cha One Fm cha Nairobi, Kenya na Bernsoft Interactive Present ameanzisha kampeni iitwayo PAMOJACONJE2012 INITIATIVE ili kumchangia fedha bondia wa zamani Congestina Achieng aliyewehuka.

Kupitia Facebook, Nonini ameandika:

“Ni initiative imeanzishwa na Nonini ku support Congestina Achieng boxer wetu wa nguvu! Kuna ile story that ran on TV and is on Newspapers all over about her current Health.The Initiative is very Transparent because we have blessings of Conje’s Dad Clement Adala and the sister who currently lives with her Caroline Adala. They are Signatories to the Account that has been opened at Family Bank.

No comments:

Post a Comment