Thursday, September 13, 2012

Ziara Ya Prince Williams na Mkewe Cathrine


Prince William na mkewe Catherine  walipewa mapokezi wanayostahili pindi walipowasili nchini Singapore  mnamo siku ya Tuesday  siku waliyoanza ziara ya siku ya kuzunguuka  kusini mashariki mwa Asia na Pacific ya kusini
Wawili hao wenye mvuto wamo katika maadhimisho ya miaka 60  ya   anniversary ya malkia  Elizabeth na mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege moja kwa moja  akaelekea katika viunga vya bustani ya maua ya Singapore Botanical Gardens  mahali ambapo walipewa zawadi ya ua nono aina orchid ambalo chotara . lakini pia katika bustani hiyo Prince Williams alipata kumbukumbu ya mamake mpenzi pale alipooneshwa ua aina hiyohiyo ya Orchid lililopewa jina la mamake mzazi  Princess Diana



Catherine akiwa na ua walilopewa kama zawadi ya jina lao! ni raha! ua chotara zuriiii

                 


                            hili limepewa jina la marehemu Princes Diana


                                 kwa pamoja wakiliajabia! lina afyaje?



                                   mbele ya ua la Princess Diana marehemu



                   inawezekana ushaliona. lakini kwa ukaribu ndivyo linavyoonekana!



itifaki imezingatiwa! shurti kukubali na kujiorodhesha kua ulikua hapo! baba akimtazama mama!



raha mno kama mapenzi bado yako juu, ona wanavyo pendeza hata wakiwa wamechomoza katika maua!



wawili hao wanafanya ziara na upekee katika harakati za kutafuta mtoto, na Prince William ameshatamka anataka watoto wawili.


William na  Catherine wanaondoka leo nchini  Singapore. Na moja kwa moja wataelekea jirani na Singapore nchini  Malaysia, ambako watatembelea mji mkuu wa Kuala Lumpur na  Borneo's Sabah state  kuanzia leo 13- hadi 15.
 Wawili hapo baadae wataelekea katika visiwa vya  Solomon  mnamo September 16-18  kabla ya kuhitimisha watakaa Tuvalu September 19

No comments:

Post a Comment