Maandamano
ya Waislamu yameenea sehemu nyingi duniani wakipinga filamu iliyotengenezwa Marekani
na inayomkashifu Mtume Muhammad, ambapo polisi wa Cairo wametumia mabomu ya
machozi kutawanya waandamanaji hao.
Rais wa
Muhammed Mursi wa Misri ametoa baraka za kufanyika kwa maandamano ya amani
lakini akasema ni kinyume kuwaua raia na kushambulia balozi. "Kutoa maoni,
uhuru wa kuandamana na kutoa misimamo ni jambo ambalo linakubaliwa lakini
pasipo kuharibu mali na balozi." Amesema Rais Mursi kupitia televisheni ya
nchi yake huku pia akilaani mauaji ya balozi wa Marekani nchini Libya na
kuahidi kulinda wageni.
Wizara ya
afya ya Misri imesema watu kumi na tatu wamejeruhiwa katika maandamano hayo
ambapo waandamanaji wameshusha bendera ya Marekani na kuichoma na kisha
kupandisha bendera nyeusi.
Serikali ya
Misri imetoa wito kwa raia wake kurejesha amani huku pia ikiikosoa filamu hiyo
ambayo imeleta hasira nchini Libya na kusababisha vifo vya raia wanne wa
Marekani akiwemo Balozi Chris Stevens mjini Benghazi.
Katika
taarifa ya baraza la mawaziri iliosomwa na Waziri Mkuu Hisham Qandil , uongozi
wa nchi hiyo umesema filamu hiyo imemdhalilisha Mtume Muhammad na pia imekiuka
maadili. "Tunawaomba wananchi wote wa Misri kueleza hasira zao kwa
amani," imeeleza sehemu ya tamko hilo.
Cairo Misri
Maandamano
ya kupinga filamu hiyo sasa yanaendeela kuenea katika nchi nyingine za
Kiislamu, ikiwemo Morocco, Sudan na Tunisia.Mjini Tunis polisi nao wamelazimika
kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji.
Mjini Sanaa,
Yemen, waandamanaji wenye hasira na filamu hiyo wamepambana vikali na polisi
wakati wa maandamano yao nje ya ubalozi wa Marekani.
Filamu hiyo
ambayo imesababisha machafuko na maandamano imeandaliwa na raia wa Marekani
mwenye asili ya Kiyahudi ambaye anauelezea Uislamu kama kidonda ndugu na
kumkashifu Mtume Muhammad .
Maandamano Libya
Wakati huo huo Marekani imetuma meli na manowari
nchini Libya baada ya balozi wake kuuawa huku pia ikiamini kwamba shambulio
hilo lilitekelezwa na al-Qaida na si raia wa kawaida.
iasi ya
askari 50 wamepelekwa mjini Tripoli kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika
ubalozi wake huku pia ikianza kuwaondoa wafanyakazi wake katika mji wa
Benghazi.
Rais Barack
Oboma wa Marekani ameitaka Libya kuimarisha ulinzi lakini pia akitaka hatua
zaidi kuchukuliwa kwa wote waliohusika na mauaji hayo.
Katika
taarifa yake hapo jana waziri wa mamabo ya nje wa Marekani Hillary Clinton
alisema mashambulizi hayo yalifanywa na kundi dogo na si raia wala serikali ya
Libya.
Maafisa wa
Marekani wanachunguza tukio hilo lakini wakiamini kwamba huo ulikuwa mpango wa
Al qaeda ambao wametumia maandamano kulipiza kisasi wakati wa kumbukumbu ya
septemba 11.
Marekani
imeendelea kuwaonya raia wake katika mataifa kadhaa kuepuka kukaa katika umati
mkubwa lakini inaimarisha ulinzi katika balozi zake zote.
Na Rais wa
Afghanistan Hamid Karzai amelazimika kusitisha ziara yake nchini Norway
akihofia ghasia zinazoweza kutokea kutokana na filamu hiyo.
No comments:
Post a Comment