Tuesday, August 21, 2012

Rihhanna a.k.a Robyn Fenty amuenzi mamake Mzazi (MONICA)


                                                                    Mama na mwana

Rihhana ni mwenye kukumbuka fadhila na kushare kile alichonacho na wapendwa wake, hivi karibuni alimpa mama yake mzazi Monica Braithwaite kile alichoona kinamfaa, na hii ilikua ni katika mahojiano na Oprah Winfrey ,zawadi hiyo ni nyumba ya haja yenye vyumba vitano mpya kabisa kwa heshima ya mama yake , nyumba ambayo iko eneo alikokulia  ,Barbados.



                      Hapa Rihanna anamuandaa mamake kupokea habari njema!



    Huwezi amini mansion hii ni yangu? you! Rihanna? me? oh myGod! mama alizuia pumzi zake



                     Mpyaaaaaaaaaaa, kwa mbele na kwa pembeni full mijiua





                         Kuzaa kuzuri jamani, kwa nyuma, mama kapewa sehemu ya kujiachia







                           Kiukweli Rihanna ali stahili hugg,! oh Mama! mama alichanganyikiwa kwa zawadi njema na kumtazama tu mwanawe! na alimwambia alitaka kumpa zawadi hiyo muda mrefu tu!



         Mama bi Monica akafanya ukaguzi wa nyumba yake mpya, mbele  ni aunt yake Rihanna!



                                Nyumba yao ya zamani Rihanna huko Barbados




                   Rihanna akimuonesha Oprah Maisha alikoanzia, ameishi hapo kwa miaka 11



             Baada ya hapo alimwagika machozi! why? ungana nami hapo chini!



Machozi hayo ni baada ya kurejelea yale yalotokea mnamo mwaka 2009, Rihanna alilielezea tukio hilo kua  lilikua la  kufadhaisha na la kinyanyasaji mno ambalo lilisababisha ampoteze rafikiye kipenzi
Na kueleza kua tangu katazo la kumtaka Chris asimkaribie Rihanna liondolewe mnamo February 2011  , basi wamekua wakijishughulisha juu ya suala la urafiki wao na wamekua karibu  na wanaonana sana tu kama mwezi ulopita walikua  St Tropez.na hawawezi kuubadili ukweli kua wao ni marafiki wa karibu ingawa ni ngumu kujiachia kwa  mpenzi wake wa zamani kwasababu hisia zake bado zinakinzana. Na mbaya zaidi bado anampenda. Na mtu asipozijua hisia zake basi anaweza kufanya makosa mengi mno!
Rihanna amainisha kua kuonana kwao si kimahaba kwani Chris tayari ana mpenziwe ambaye ni model Karrueche Tran, na yeye anabaki kua single na kumbukumbu za mahaba yao bado zinajirudia kichwani mwake kila uchao na anadhani Chris Brown  ndiye wake wa maisha na yeye ndiye aliyeanza naye.


Lakini katika wakati huu sasa! Rihanna anaonesha kweli amekomaa kwani anasema wakati ajali ilipotokea ya kupigwa na mpenzi wake, walikua bado wadogo walipoangukia mapenzini, wakaenda nayo mbio,na kujisahau wao wenyewe.
Na il kua na amani na kuvunja unyanyasaji ameamua kumsamehe baba yake  na kutengeneza upya uhusiano wao na baba huyo, Ronald Fenty.kwani mwanzo alikua na hasira naye , kutokana na mambo kadhaa yaliyotukia utotoni mwake na hakuweza  kutofautisha mume na baba! Na akatanabahisha hasira zake zatokana na unyanyasaji wa baba kwa mamake bi Monica.
Wazazi wa Rihanna walitengana miaka miwili kabla Rihanna ahajaondoka Barbados wakati huo Riri alikua na miaka  16. Rihana ameeleza kua tabia ya babake iliitenga familia yao. Japokua hakutaja makosa halisi! Na hii inathibitisha msamaha halisi kwa babake, na kwamba amejifunza kutoka kwa Chris Brown, na kwamba sasa maisha yaendelee baada ya miaka 3 ya kugubikwa na scandal ya kupigwa na mpenziwe wa zamani.
Naye anasema nami namnukuu 'I have to move on,' na . 'I have forgiven him. It took me a long time. I was angry for a long time.' Wow nimemsamehe,ingawa imenichukua muda mrefu! Maisha inabidi yaendelee! Nampenda sana! Kikubwa  ninachofurahia ni kwamba Chris ana amani kwa sasa, najali, ina maana kwangu kwamba ana amani tena.
Na ametoa wito kwa watu wanaomshangaa kumsamehe alompiga! Anasema hawezi kuzuia hisia zao, ilikua kitu mbaya wao kua na hasira ilikua sawa kwa kilichotokea, lakini nimemsamehe!

No comments:

Post a Comment