Rais wa Africa kusini Jackob Zuma
Kamisheni inayojishughulisha na masuala ya usawa wa kijinsia nchini Africa Kusini walipokea malalamiko kutoka kwa chama cha Democratic Alliance kuhusiana na rais Jacob Zuma kutokana na maneno ama nasaha alizozitoa dhidi ya wanawake akiwa katika mahojiano hai kwenye television ya SABC3 nchini humo.
Kamisheni hiyo inashughulikia malalamiko hayo na kutolea ufumbuzi.
Zuma alitoa maoni yake wakati wa mahojiano na Dali Tambo katika show yenye jina la watu wa Africa Kusini,kipindi hicho kilirushwa siku ya jumapili na interview hiyo ilifanyika nyumbani kwa rais huyo huko Inkandla.
Lakini pamoja na hayo yote ama pengine! Sintofahamu hiyo imetokea wakati wa harusi ya bintiye kipenzi! Ndio, kwani Rais Zuma hivi karibuni alipata mkwe kutoka kwa bintiye kipenzi Duduzile na mkwe huyo ni Lonwabo Sambudla,na hisia za raisi Zuma alizieleza wazi kua anaona fahari juu ya bintiye kwa hatua aliyofikia.
Na sababu kuu ya furaha yake ni kwamba anadai kua hakupenda kukaa na binti amabaye hajaolewa! Kwasababu kua single katika jamii ni tatizo,ila anafifikiri iko dhana miongoni mwa watu wanaodhani kua single ni kitu kizuri,kiukweli hali hiyo si nzuri asilani, na ni ajabu!
Anasema kwa mwanamke unapaswa kua na watoto! Watoto ni muhimu kwa mwanamke na si muhimu tu bali ni mafunzo ya ziada kwa mwanamke pindi azaapo na kua mama.
Chama hicho cha Democratic Alliancekinautazama usemi wa rais Zuma kama umekaa kimahaba zaidi na una jambo ndaniye dhidi ya wanawake .
Wimbo alochagua binti huyo katika harusi yake ni wa Shania Twain uitwao from this moment on!
Shuhudia kidogo harusi hiyo kati ya Duduzile na Lonwabo Sambudla.
baba na mwana, baba Zuma wakati anamuingiza kanisani Bintiye
Maharusi Duduzile na bwana harusi Lonwabo
Busu la Kwanza
na busu hilo hapo juu shurti upitie hatua hii ya kuuza uhuru wako, ndipo utabusiwa!
Meza kuu!
Jikeki lilikuwepo kukamilisha furaha yao!
baada ya hapo furaha ilitawala!!!!
Rais Zuma hakusita kuonesha furaha yake kwa tukio hilo kubwa
kifamilia zaidi!
huu ndo unyayo wa siku ya harusi yake
kama walivyo wa Ghana na Nigeria , South Africa nao huwa na harusi ya kimila, maharusi hawa nao walipitia hatua hiyo na ndivyo wanavyoonekana!
akiwa katika vazi la kitamaduni bi harusi Duduzile
tusubiri kusikia hatma ya wanaharakati hao juu ya kauli ya Rais Jackob Zuma dhidi ya wanawake.
No comments:
Post a Comment