Wanamichezo watano waliohudhuria michezo ya Olympic jijini London Uingereza kutoka nchini Cameroon, wanasema wanataka ukimbizi kuendelea kubaki nchini Uingereza baada ya kutoweka katika kijiji cha Olympic wiki iliyopita.
Wanamichezo hao wanaume watano wote wakiwa ni mabondia wameiambia BBC kuwa waliondoka katika kijiji cha mashindano ya Olympic mashariki mwa London baada ya kutishiwa na maafisa wa juu wa timu ya Olympic ya Camerron, kuwa wangeadhibiwa iwapo wangeshindwa katika mashindano hayo kwa kuondoka mikono mitupu bila ya kupata medali.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa mabondia hao THOMAS ESSOMBA amesema wanataka kubaki nchini Uingereza ili kuendeleza taaluma yao ya kimichezo katika ndondi .
Essomba ameenda mbali zaidi na kudai kuwa viongozi wa msafara wao waliwatisha kwa kuanza kuwaamuru wale waliokuwa tayari wameshiriki michezo mingine na kushindwa kusalimisha hati zao za kusafiria.
No comments:
Post a Comment