Mwanama mwenye historia nzuri katika medani ya habari na mahojiano mkubwa Oprah, hivi karibuni amefanikiwa kumtia katika kumi na nane zake mrembo Rihanna katika show yake OWN network ,show ya Oprah ambayo inaingia katika ukurasa mwingine sasa na kuwashika watazamaji na washabiki wa bi mkubwa huyo mahiri katika fani ya utangazaji na mahojiano
Tumemshuhudia binti wa miaka 24 akishusha mvua ya machozi wakati alipokua akimzungumzia Chris Brown na mwisho wa mapenzi yao , lakini kwa sasa RIRI anaona kama historia tu , na mwimbaji huyo anakubali kua mahusiano yao baada ya miaka 3 bado ana mhitaji kwani ana mmiss.
Kwa muujibu wa mahojiano hayo ya hivi karibuni this latest, Rihanna hahuzunishwi tu na mwisho wa mapenzi yao! Lakini anamkumbuka Breezy kila iitwapo leo .
Na Rihanna anafunguka kile kinachomfanya amkumbuke kwa mengi , moja ni zile kumbukumbu nzuri walizokua nazo, mambo yenyewe si makubwa sana! Ni kama vile vyumba vya hotel,maeneo waliyotembelea,chochote kizuri,muziki walosikiza pamoja, nyimbo, na ana mkosa kwa nyakati hizo!
Na Oprah akamchombezea Chriss “She talks a lot, a lot, a lot about you know who, Mr. Chris Brown.”
Lakini pamoja na hayo, Riri hayuko na Breezy, RiRi aeleza anamtaka mwanamume wa aina gani ajaye :
Hapa namnukulu "I know what I want… RIRI anajua anachokitaka, kama itatokea tena anamtaka mwanamume anayempenda,atakaye nijali,atakayenithamini lakini anapaswa kuijua thamani yangu ili kunithamini kwasababu RIRI mwenyewe anaijua thamani yake hivyo anataka kuheshimiwa . kama hiyo haitoshi anataka muda wa kujiachia mpaka baasi , anataka mtu atakayemfanya acheke muda wote, anapenda kucheka kuliko kitu chochote kwasababu ana kila kitu hivyo alivyovitaja anavihitaji zaidi na anachotaka kwasasa ni mshkaji, ama mwenza wa kufurahi naye
Pamoja na yote yalotokea Rihanna na Chris walikua na uhusiano wa muda mrefu wenye mahaba ya dhati , haya twasubiri nini Rihanna ataelezea juu ya mshkaji wake huyo wa zamani maan inaonekana yuko kichwani mwake na sasa anamuongelea.
Pamoja na yote yalotokea Rihanna na Chris walikua na uhusiano wa muda mrefu wenye mahaba ya dhati , haya twasubiri nini Rihanna ataelezea juu ya mshkaji wake huyo wa zamani maan inaonekana yuko kichwani mwake na sasa anamuongelea.
No comments:
Post a Comment