Friday, February 8, 2013
Askari polisi na Dereva wa Bajaji Wakamata MAHELA ya VODACOM.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL KATIKA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA MAREKANI
Wednesday, February 6, 2013
KESI YA UBAKAJI YAANZA KUSIKILIZWA INDIA
HII NI KWA TAARIFA YAKO TU!

Kesi ya watu
watano wanaotuhumiwa kumbaka na kumuua mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini India
Desemba mwaka jana imeanza kusikilizwa. Rafiki wa mwanamke huyo, ambaye ni
mhandisi wa komputa mwenye umri wa miaka 28, alitoa ushahidi katika kesi
iliyosikilizwa kwa siri, na kuwatambua watuhumiwa hao na basi ambamo uhalifu
huo ulitendeka. Inadaiwa kuwa wanaume sita walimshambulia yeye na mwanamke
wakiwa ndani ya basi wakirejea nyumbani. Mwanamke alibakwa mfululizo na kuteswa
kwa kutumia nyundo, na alifariki wikimbili baadaye kutokana na majeraha. Tukio
hilo lilisababisha maandamano ya nchi nzima, na mjadala juu ya namna wanawake
wanavyotendewa nchini India. Siku ya Jumapili, India ilianzisha adhabu kali
dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia--- kwa kuweka kifungo kisichopungua miaka 20
kwa ubakaji, na adhabu ya kifo kama ubakaji huo ulisababisha kifo. Mtuhumiwa wa
sita anashtakiwa tofauti kwa kuwa yeye ni mtoto.
Ndoa za jinsia moja zakipasua chama tawala Uingereza

waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.
Bunge la Uingereza limepiga kura kuidhinisha mswada wa sheria inayohalalisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja -- licha ya mpasuko katika chama tawala cha waziri mkuu David Cameron. Mswada wa sheria hiyo, ambao bado una safari ndefu ya kuwa sheria, ulipita kwa kura 400 dhidi ya 175. Shinikizo la Cameron kuruhusu watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kuoana nchini Uingereza na Wales, limesababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya chama chake cha Conservatives, lakini limeungwa mkono na chama cha upinzani cha Labour
Monday, February 4, 2013
Mgombea urais Paraguay afariki dunia
Subscribe to:
Posts (Atom)



