Monday, February 4, 2013
Mgombea urais Paraguay afariki dunia
Mgombea wa urais nchini Paraguay, Lino Oviedo amefariki dunia.
Kikazi zaidi mwanajeshi mstaafu Lino Oviedo
Lino Oviedo amekufa katika ajali ya helcopter
Katika harakati zake za kampeni
Wafuasi wake wakiwa hawaamini!
Ni vilio tupu!
Mgombea wa urais nchini Paraguay, Lino Oviedo amefariki dunia katika ajali ya helikopta. Oviedo, mwanajeshi mstaafu aliyekuwa na cheo cha Jenerali, alikuwa akisafiri kuelekea kwenye kampeni kaskazini mwa nchi hiyo, akiwa pamoja na mlinzi wake. Rubani wa helikopta hiyo alitoa taarifa ya hali mbaya ya hewa kabla ajali hiyo haijatokea na kusababisha vifo vya watu wote watatu waliokuwemo ndani. Oviedo alisaidia kuongoza mapinduzi miaka 24 iliyopita na kumuondoa madarakani dikteta Alfredo Stroessner ambaye alikuwa madarakani tangu mwaka 1954.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment