Thursday, February 28, 2013

Clouds FM yatwaa tuzo ya 'SuperBrand' mara 4 mfululizo


Mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga wa kwanza kulia akikabidhiwa cheti cha kuthibitisha kua Clouds Fm ni “SUPERBRAND” kwa mara ya nne mfululizo!.




Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (kati) pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer kwa pamoja wakimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga kwa Couds Fm redio kuibuka na tuzo hiyo ya ubora kwa mara ya tatu mfululizo. Tukio hilo lilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya Clouds Media Group kupitia kituo chake cha Redio Clouds Fm, kwa mara nyingine tena kimeibuka mshindi na kukabidhiwa rasmi tuzo ya kuwa kituo bora nchini kwa Mwaka 2013/2014 kupitia tuzo za Ubora wa Makampuni yani “SUPERBRAND”
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, JOSEPH KUSAGA, amesema ushirikiano mzuri uliopo baina ya Wafanyakazi pamoja na Uongozi kwa ujumla umechangia kwa kiasi kikubwa Clouds Fm kuwa SUPERBRAND kwa miaka mine mfululizo sasa.

Joseph  Kusaga  amesema katika kuhakikisha kuwa Clouds fm inaendelea kuwa kituo bora nchini mitambo yake itaendelea kuboreshwa zaidi na kuhakikisha kuwa matangazo yake yanafika nchi nzima ifikapo Juni mwaka huu.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji na Uwezeshaji, DK MARY NAGU, ameeleza kuridhishwa kwake na mchango ambao umekuwa ukitolewa na Kampuni Binafsi nchini katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali.

Kwa mara ya nne mfululizo Clouds Fm, imeendelea kuwa Kituo bora cha Redio nchini kupitia tuzo za Makampuni bora yaani “SUPERBRAND” kutokana na ubora wa Vipindi vyake vyenye ubunifu wa hali ya juu.


No comments:

Post a Comment