Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Sista Rosaria Gargiulo wa Shirika la Masista Waabuduo Damu ya Yesu alipowasili kwenye Kijiji cha Matumaini kinacholea watoto yatima eneo la Kisasa, Dodoma leo mchana Februari 7, 2013. Katikati ni Padre Vincent Boselli anayesimamia mradi wa kijiji hicho.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (wa pili kulia) akiwa amembeba mtoto Consolatha kwenye shule ya awali ya Kijiji cha Matumaini kinacholea watoto yatima eneo la Kisasa, Dodoma . Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, wilaya ya Dodoma Mjini, Bi. Fatuma Mwenda na (kushoto) ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo, Bi Salome Kiwaya.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimwangalia mtoto wa kiume aliyezaliwa leo saa 11 alfajiri (Februari 7, 2013) na Bi. Fatma Mohammed kwenye kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini. Bi. Fatma ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nzuguni, alisema atamwita mtoto huyo Pinda kwa sababu mama Pinda amekuwa mtu wa kwanza kumjulia hali.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa amembeba mtoto wa kiume , kwenye kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini. Mama wa mtoto huyo, Bi. Fatma Mohammed alisema atamwita mtoto huyo Pinda kwa sababu Mama Pinda amekuwa mtu wa kwanza kumjulia hali.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa amembeba mtoto Cyprian (doto) mmojawapo wa mapacha wanaolelewa katika kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini wakati alipotembelea kijiji hicho Februari 7, 2013. Pacha mwingine (kulwa) Christian) amebebwa na Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Dodoma, Bi Salome Kiwaya. Kushoto ni Pd. Vincent Boselli akielezea jinsi watoto hao wenye miezi mitatu walivyofikishwa kituoni hapo wakitokea Morogoro.
Baadhi ya watoto wa Kijiji cha Matumaini wakiangalia zawadi walizopelekewa na Mama Tunu Pinda .
Neema Ntandu (wa tatu kushoto) ambaye ni mmojawapo wa watoto watatu waliokuwepo wakati Kijiji cha Matumaini kikianzishwa mwaka 2002, akimkabidhi zawadi ya sanamu ya Bikira Maria, Mama Tunu Pinda ambayo imetengenezwa na watoto wa kijiji hicho wakati Mama Pinda alipotembelea kijiji hicho .
No comments:
Post a Comment