Papa Benedict amefanya misa yake ya mwisho hadharani kabla
ya kujiuzulu rasmi hapo kesho, kitendo kama hicho kilifanyika katika Kanisa
Katoliki miaka mia sita ilyopita.
Amewaambia maelfu ya watu waliokusanyika katika viwanja vya
Mtakatifu Petro huko Vatican kwamba alikuwa anafahamu uzito wa aamuzi wake
lakini amefarijika kutokana na imani yake kwa Mungu na Kanisa Katoliki.
Papa aliwaambia mamia ya waumini waliofika kushuhudia misa
yake kuwa anafahamu vyema athari za umauzi wake lakini alikuwa na amani kwa
sababu ya imani yake kwa Mungu na kanisa.
Mara kwa amara waumini walishangilia hotuba zake akisema
kuwa alihisi kupotewa na nguvu katika miezi ya karibuni na kumtaka Mungu
kumsaidia katika kufanya uamuzi huu.
Pia alisema kuwa atamuombea mrithi wake atakayechaguliwa
katika wiki chache zijazo.
Rozari zenye taswira ya Pope Benedict wa 16
Masista wakiwa na bango lenye neno la kitaliano lenye maana ya asante kwa kiswahili!
Makardinali na maaskofu ibadani
akipita hapa na pale baada ya ibada.
Pope akibariki.
kwa kawaida katika viwanja vya basillica hufurika!
No comments:
Post a Comment