Mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester City
wameandikisha ushindi mkubwa dhidi ya mabingwa wa ulaya Chelsea na hivyo
kufufua matumaini yao ya kuhifadhi kombe hilo kwa mwaka wa pili, licha ya
kukabiliwa na upinzani mkali kutoka wa vinara wa ligi hiyo kwa sasa Manchester
United.
Mechi hiyo iliyokuwa na mashambulizi na kila aina ya vivutio
baina ya timu hizo zinazomilikiwa na matajiri wawili tofauti,imemalizika kwa
ushindi wa Man City wa mabao mawili kwa bila.
Mabao ya kipindi cha pili ya Yaya Toure na Carlos Tevez
yalitosha kuizamisha Chelsea, na kufufua matumaini ya Man City, kutetea taji
lao ambalo sasa linaonekana kuwa mikononi mwa majirani zao Manchster United
wanaoongoza ligi wakiwa na tofauti ya point 12.
Mapema kipindi cha pili, Chelsea, walipata penat baada ya
Demba BA, kuangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Man City, Joe
Hart, lakini penat iliyopigwa na nahodha wa Chelsea, Frank Lampard,
ilipanguliwa Joe Hart na kuamsha mashambulizi zaidi ya Manchester City.
Yaya Toure kunako dakika ya 63 alipenyeza shuti la wastani
pembeni mwa lango la Chelsea na kuwafanya
Manchester City, kuongoza kwa bao
moja kabla Chelsea, kufanya juhudi za kutaka kusawazisha lakini wakajikuta
wanoangezwa bao la pili maraidadi kabisa lililofungwa na Carlos Tevez ambaye
aliingia akitokea benchi,huku likiwa bao lake la kwanza baada ya mechi sita
alizocheza bila kuifungia timu yake.
Kwingineko,katika mchezo mwingine , Newcastle wakiwa
nyumbani,walitoka nyuma baada ya kufungwa bao la mapema na kuchomoza na ushindi
wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Southampton.
Mabao wa Newcastle yamefungwa na Musa Sisoko,Papis Demba
Cisse,Yohan Cabaye aliyefungwa kwa mkwaju wa penati huku bao la nne watakatifu
au Southampton wakijifunga.
Mabao ya Southampton yalifungwa na Morgan Scheneiderlin
dakika tatu tu baada ya mchezo kuanza huku bao la pili likifungwa na Rickie
Lambert.
No comments:
Post a Comment