Maonyesho ya filamu mia kadha kutoka sehemu mbali-mbali za
Afrika na Wafrika walioko ng'ambo, zitaoneshwa katika tamasha kubwa ya
utamaduni wa Afrika ambayo inaanza Burkina Faso Jumamosi.
Maonyesho hayo ya Panafrican Film and Television Festival ya
Ouagadougou (FESPACO) yanafanywa kila baada ya miaka miwili.Tuzo kubwa kabisa -
Stallion of Yennenga - hupewa filamu ambayo inaonesha maisha halisi kabisa ya
Afrika.
Filamu 20 za habari hasa kutoka Morocco, Algeria, Angola na
Senegal zinagombea tuzo hiyo.Ingawa Misri haikujiandikisha kwenye mashindano
hata hivyo itaonesha filamu ya msanii wa Misri, Khaled Sayed, iitwayo
"Stories from Tahrir".Inaangalia changamoto ambazo Wamisri wanakabili
wanapogombania uhuru.
No comments:
Post a Comment