Reeva Steenkamp
Kampuni moja ya televisheni ya Afrika Kusini inasema
itasonga mbele na mpango wake wa kutangaza kipindi kinachomuonesha Reeva
Steenkamp, mchumba wa mawanariadha mlemavu, Oscar Pistorious.
Msichana huyo alipigwa risasi na kuuwawa nyumbani mwa Bwana
Pistorious siku ya Alkhamisi na mwanariadha huyo sasa ameshtakiwa kwa mauaji
yake.Alipouwawa Reeva Steenkamp alikuwa anakaribia umaarufu mkubwa.
Mrembo huyo aliyekuwa na umri wa miaka 29 alikuwa ashiriki
kwenye kipindi cha Tropical Island of Treasure ambacho kinge tayarishwa nchini
Jamaica.Katika hatua ambayo itaonekana na utata shirika la habari la SABC
limeamua kuonesha kipindi kimoja tayari kimesharikodiwa, licha ya mauaji ya
Reeva Steenkamp.
Mtayarishi wa kipindi alisema kipindi cha juma hili kitakuwa
kumbu-kumbu ya Reeva Steenkamp.Wakati huohuo mabango yaliyokuwa mabara-barani
yanayomuonesha mchumba ake, Oscar Pistorius, yanabanduliwa.Pistorius bado
anazuwiliwa na polisi baada ya kuifikishwa mahakamani Ijumaa.
Ombi lake la kutaka kuachiliwa kwa dhamana litasikizwa
Jumaane
No comments:
Post a Comment