Wednesday, February 6, 2013

Ndoa za jinsia moja zakipasua chama tawala Uingereza




waziri mkuu  wa Uingereza David Cameron.

Bunge la Uingereza limepiga kura kuidhinisha mswada wa sheria inayohalalisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja -- licha ya mpasuko katika chama tawala cha waziri mkuu David Cameron. Mswada wa sheria hiyo, ambao bado una safari ndefu ya kuwa sheria, ulipita kwa kura 400 dhidi ya 175. Shinikizo la Cameron kuruhusu watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kuoana nchini Uingereza na Wales, limesababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya chama chake cha Conservatives, lakini limeungwa mkono na chama cha upinzani cha Labour

Watu wa jinsia moja wakivalishana pete!

No comments:

Post a Comment