Najua unaweza kua huioni vyema! subiri
Hii ni hatari! kwa afya! imetokea wapi?
BAADHI ya wananchi ambao ni watumiaji wa vinywaji baridi
Jijini Mbeya wameyalalamikia baadhi ya makampuni yanayohusika na utengenezaji
wa bidhaa hizo kwa kutozingatia usalama wa watumiaji.
Malalamiko hayo yamekuja kufuatia hivi karibuni mwananchi
mmoja aliyoomba kuhifadhiwa jina lake kununua soda aina ya Tonic Water
inayotengenezwa na kampuni ya Coka kukutwa ikiwa na karatasi la pombe kali aina
ya Vodka.
Soda hiyo ikiwa mpya bila kufunguliwa ilikutwa katika duka
moja eneo la Simike baada ya mteja huyo kuuiwa kwa lengo la kiutuimia lakini
kabla ya kuifungua ndipo laipogundua uchafu huo.
Kufuatia hali hiyo Mwandishi wa stori hii alipewa taarifa na mhusika ambapo walienda
moja kwa moja hadi kiwandani Coka eneo la Iyunga Jijini Mbeya na kupokelea na
Meneja mauzo wa wilaya(Area sales Manager)
Baada ya kupokelewa na kuelezwa hali iliyotokea meneja huyo
aliwapeleka waandishi kwa kitengo cha ubora wa bidhaa ambao bila woga walisema
tuwaachie soda hiyo baada ya kuridhishwa kuwa ni mpya na inatoka kiwandani hapo.
Walidai waachiwe soda hiyo ili kuifanyia uchunguzi wa
kimaabara katika uchunguzi utakafanyika kwa wiki moja hali iliyoleta sintofaham
kwa walalamikaji huku wakihoji uchunguzi gani ufanyike ili hali uchafu
unaonekana.
Aidha walidaikuwa pamoja na kukataliwa kubakishwa kwa soda
hiyo walisema mlalamikaji hatanufaika na chochote ikiwa na kiwanda kutoathirika
na tatizo hilo licha ya kuhusika na kuzalisha bidhaa yenye uchafu.
Hali kama hizo zimekuwa zikiwaathiri watumiaji wa vinywaji
hivyo hasa wanaotumia nyakati za usiku
muda ambao si rahisi kwa mteja kugundua hali ya uchafu katika vinywaji.
Hata hivyo mhusika aliyepatwa na janga la soda hiyo kutoka
kiwanda cha Coka aliiomba mamlaka zinazohusika kufuatilia hali ya usafi wa
vifaa vya kubebea vinywaji hivyo kabla ya kupelekwa sokoni kwa watumiaji ili
kunusuru afya za wananchi.
No comments:
Post a Comment