Wananchi
hususani wanaoishi na Virusi vinavyosababisha UKIMWI nchini UGANDA,
wamepokea kwa furaha kubwa habari ya kuwa Taifa hilo litakuwa linaanza kutengeneza
dawa za kupunguza makali ya UKIMWI.
Wakizungumza
kwa nyakati Tofauti wananchi hao wamesema kuwa kitendo cha Taifa hilo kuainisha
mikakati ya kutengeneza dawa za ARV,
kitaleta nafuu kubwa kwa waathirika wa maambukizi ya HIV kwa kuwa wana matumaini hata bei ya vidonge hivyo itapungua kwa
kiasi kikubwa.
ALLAN RWASSA ni miongoni mwa Waathirika wa UKIMWI nchini humo.Baada ya hapo Bwana RWASSA akatoa ushauri nasaha kwa
wananchi wanaoishi na Virusi vya UKIMWI nchini
UGANDA, juu ya umuhimu wa kuzingatia
matumizi ya dawa hizo.
No comments:
Post a Comment