Nigeria ndio mabingwa wapya Kombe la Afrika 2013 baada ya
kuilaza Burkina Faso 1-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa katika uwanja wa
taifa, jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Nigeria mabingwa wapya Afrika 2013,yailaza Burkina Faso 1-0
katika mchezo wa fainali nchini Afrika Kusini.Ni shangwe na vigelegele katika
miji mbalimbali nchini Nigeria baada ya timu yao ya The Super Eagles, kuibuka
mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mbio za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika zilizoanza tarehe
19 Januari zimehitimishwa, Jumapili, tarehe 10 Februari kwa Nigeria kuibuka
bingwa wa fainali za mwaka 2013 barani Afrika.Bao la mchezaji Sunday Mba
alilofunga katika dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza cha mchezo mjini
Johannesburg, ndilo lililowahakikishia The Super Eagles, Nigeria kuwa mabingwa
wapya.
Mchezo huo ulianza kwa kasi, timu zote mbili zikishambuliana
kwa zamu. Hata hivyo Nigeria ndiyo walionekana kutawala zaidi mpambano huo na
kukosa magoli kadha ambayo yangeipa ushindi mnono Nigeria.
Vijana hao wa Super Eagles, wamekuwa wakiimarika kila hatua
ya mashindano hayo, hasa baada ya kufuzu kutoka katika makundi. Ni katika hatua
ya makundi ambapo mabingwa watetezi, Zambia walitolewa na kuachia kombe hilo
kufukuziwa na timu nane zilizoingia robo fainali, na hatimaye timu mbili
zilizotinga fainali, Nigeria na Burkina Faso.
Emmanuel Emenike aliibuka mfungaji bora wa mashindano hayo
na kupata kikombe,na kiatu cha dhahabu huku Moses Victor akiwa mchezaji bora wa mechi kati ya
Nigeria na Burkina Faso.Mechi hiyo ya fainali ilihudhuriwa na Rais Jacob Zuma
wa Afrika Kusini, akiwa mgeni rasmi, akiambatana na rais wa Fifa Sepp Blatter
na rais wa CAF, Issa Hayatou.
The Super Eagles pia waliahidiwa zawadi kem kem, zikiwemo
fedha taslim kwa kocha na wachezaji, hata kabla ya kutwaa ubingwa.Hii ni zawadi
kubwa kwa kocha wa Super Eagles, Stephen Keshi ambaye mwaka 1994, wakati
Nigeria ilipotwaa ubingwa wa Afrika, alikuwa nahodha wa timu hiyo katika
fainali zilifanyika nchini Tunisia.
Pia Nigeria ilitwaa ubingwa mwaka 1980, wakati fainali hizo
zilipoandaliwa nchini Nigeria.Super Eagles kama ilivyo kwa timu nyingine barani
Afrika, itakuwa ikijiandaa kikamilifu kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia
zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Licha ya kushindwa katika mechi hiyo ya Fainali, mashabiki wa Burkina Faso walishangilia mitaani, na kocha wa timu yao Paul Put amesema wameipatia nchi yao heshima kubwa.
Katika ligi kuu ya Ujerumani, Bundes Liga, Mainz ilitoka sare ya goli moja na timu inayojikongoja ya Augsburg. Freiburg iliweza kuishinda kwa taabu Fortuna Düsseldorf kupitia goli lililoingizwa na Pavel Krmas katika dakika ya 87.
Licha ya kushindwa katika mechi hiyo ya Fainali, mashabiki wa Burkina Faso walishangilia mitaani, na kocha wa timu yao Paul Put amesema wameipatia nchi yao heshima kubwa.
Katika ligi kuu ya Ujerumani, Bundes Liga, Mainz ilitoka sare ya goli moja na timu inayojikongoja ya Augsburg. Freiburg iliweza kuishinda kwa taabu Fortuna Düsseldorf kupitia goli lililoingizwa na Pavel Krmas katika dakika ya 87.
No comments:
Post a Comment