Diwani wa Kata ya Kipawa Manispaa
ya Ilala, Bonnah Kaluwa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar
es Salaam leo, kuhusu awamu ya pili ya Mradi wa Mazingira Bora kwa Elimu Bora ,utakao
zinduliwa kesho katika Kata hiyo. Kushoto ni Meneja wa Mradi huo Regina Ogwai.
Mradi huo utafadhiliwa na nchi ya Marekani.
Diwani wa Kata ya Kipawa Manispaa
ya Ilala, Bonnah Kaluwa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar
es Salaam leo, kuhusu awamu ya pili ya
Mradi wa Mazingira Bora kwa Elimu Bora utakao zinduliwa kesho katika Kata hiyo.Kushoto
ni Meneja wa Mradi huo Regina Null. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Said
Fundi.
DIWANI wa
Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa amesema Kata yake inahitaji zaidi ya sh.milioni
217 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu katika Kata hiyo
iliyopo Manispaa ya Ilala.
Hayo aliyabainisha Dar es Salaam leo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa elimu katika kata hiyo na kuwa leo watazindua awamu ya pili ya mradi wa kuboresha mazingira bora ya elimu katika Kata hiyo.
Alisema katika tathmini walioifanya awali wamebaini kila shule inahitaji jumla ya sh.milioni 31 ili kupata matundu 16 ya vyoo walimu pamoja na wanafunzi katika shule zote zilizopo katika kata hiyo."Mahitaji ya vyoo hivi ni kwa shule zote saba za kata ya Kipawa zikiwemo mbili za Sekondari na tano za msingi" alisema Kaluwa.
Alisema mradi wa kwanza walifanikiwa kupata sh.milioni 155,500,000 ambapo waliweza kununua madawati 500 ya shule za msingi, 480 ya sekondari na viti 100 vya shule ya awali na kuchimba kisima cha maji katika kila shule.
Alisema katika awamu hii ya pili wamelenga kujenga vyoo na madarasa ambapo watu mbalimbali wamealikwa wakiwemo watu wa Marekani ambao wameonesha nia ya kusaidia mradi huo.Alisema awali kata hiyo ilikuwa na changamoto ya ukosaji wa maji mashuleni na madawati lakini kwa sasa kero hizo zimekwisha kutoka na ushirikiano wa wadau mbalimbali waliojitolea kuchangia maendeleo ya kata hiyo hasa katika sekta ya elimu.
Alizitaja shule hizo zilizopo katika kata hiyo ambazo zitanufaika na mradi huo kuwa ni Minazi Mirefu, Airwing, Mogo, Kipawa na Majani ya Chai.Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Said Fundi alimshukuru Diwani huyo kwa kuiwezesha kielimu kata hiyo na kupunguza changamoto zilizopo ikiwemo ya ukosefu wa maji katika shule hizo.
Kaluwa alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali wa elimu na afya pamoja na wazazi kujitokeza kwa wingi kufanikisha mradi huo wenye malengo ya kuboresha elimu ya msingi na sekondari katika kata hiyo.

No comments:
Post a Comment