Mamiss wakiwa katika picha ya pamoja.
mkao huu huwa unanipa raha sana. ni wa kiubunifu.
Bendi ya Akudo Impact wazee wa masauti ,siku ya Jumapili
tarehe 17, Februari 2013, itatoa burudani katika shindano la Taifa la kumsaka
Mrembo wa Utalii mwenye kipaji kati ya warembo 40 waliopo kambini Ikondelelo
Lodge wakijiandaa kushiriki Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13
zitakazo fanyika mwisho wa mwezi huu katika Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es
Salaam.
Katika shindano hilo la Vipaji , ambalo litafanyika katika
Ukimbi wa Jeshi wa Msasani Beach Club Jumapili kuanzia saa nane mchana ,pamoja
na Bendi hiyo ya Akudo Impact , wasanii wengine watakao tumbuiza ni pamoja na
mwanamuziki wa kimataifa Che Mundugwao, Msanii mdogo chipukizi wa muziki wa
kizazi kipya Geneous na burudani za ngoma za asili kutoka katika kundi kongwe
la Kaole Sanaa Group wakiomgozwa na
mwana dada mahili katika uchezaji wa ngoma za asili Mariam Kweji aka kalunde wa
Bongo Movie.
Shindano hilo la Vipaji ni moja ya mashindano ya awali ya
kuwania tuzo mbalimbali kabla ya Fainali kuu,ambapo washiriki wote watashindana
kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za makabila mbalimbali ya mikoa wanayo
iwakilisha. Mikoa hiyo na majina ya washiriki katika mabano ni Arusha (Rose Godwin), Dar es Salaam 1 (Sophia
Yusuph),Dar es Salaam 2(Ivon Stephen),Dar es Salaam 3 (Irine Thomas),Dodoma
(Erica Ekibariki), Geita (Hamisa Jabiri), Iringa (Debora Jacob), Kagera
1(Elline Bwire), Kagera2 (Jania Abdul),
Kagera 3(Mulky Uda), Kilimanjaro (Anna
Pogaly), Lindi (Joan John), Mtwara (Halima Hamis),Mara (Dorine Bukoni), Manyara
(Mary C. Lita), Mbeya (Diana Joachim), Mwanza (Jesca Peter), Morogoro (Hadija
Said),Tanga (Sarafina Jackson), Ruvuma 2 (Leah Makange), Tabora (Magreth
Malalle), Njombe (Pauline Mgeni), Rukwa (Anganile Rogers), Katavi (Asha
Ramadhani ), Simiyu (Flora Msangi), Shinyanga (Lightness Kituwa), Ruvuma
(Furaha Kinyunyu), Kigoma 1(Zena Ally), Kigoma 2(Rosemary Emmanuel), Pwani
(Beatrice Iddy), Singida (Neema Julius), Singida (Christina Daud),Vyuo Vikuu
(Irine Richard), Vyuo Vikuu (Hawa Nyange)
Wakizungumzia kwa nyakati tofauti shindano hilo la
Vipaji,Rais wa Miss Tourism Tanzania International Organisation ,wenye dhima ya
kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo , alisema kuwa mandalizi karibu
yote yamekamilika kuanzia ngazi za warembo hadi burudani za bendi, ngoma za
asili na muziki wa kizazi kipya. Hili litakuwa ni tukio kubwa na la kihistoria
kuwahi kufanyika Tanzania ambapo Utalii, Urembo na Utamaduni wa ngoma za asili
vitaonyeshwa kwa pamoja jukwaani, lakini kivutio cha pekee ni jinsi mabinti wa
kizazi kipya tena warembo kutoka mikoa yote ya Tanzania na vyuo Vikuu watakavyo
onyesha maajabu ya kusakata ngoma za asili kwa umahili mkubwa na wa pekee.
Shindano la Miss Utalii Tanzania mwaka huu limedhaminiwa na
wadhamini mbalimbali wakiwemo Coca Cola Kwanza Limited, Daja Salon, Mtwana
Catering Services Enterprises, Zizzu Fashion, Global Publishers, Ikondelelo
Lodge, Clouds Media Group, Tone Multimedia Group,Valley Spring na
www.misstourismorganisation.blogspot.com
Katika Shindano hili viingilio vitakuwa ni kama ifuatavyo
5,000 kwa viti vya kawaida, 10,000 kwa V.I.P 2, na 30,000 kwa V.I.P 1 pamoja na
Chakula.
No comments:
Post a Comment