VIONGOZI wa ngazi ya juu wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) wamemshitaki Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania Anne Makinda kwa wapigakura, kutokana na kitendo chake cha kushindwa
kusimamia maadili ya Bunge hilo.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo
katika viwanja wa Tandika Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam, viongozi hao
walisema kwamba Makinda ameshindwa kuliongoza bunge hilo, badala yake
anafanyakazi ya kukwamisha hoja binafsi zinazotolewa na wabunge wa upinzani
zenye lengo a kuboresha maslahi ya wananchi.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akizungumza katika
mkutano wa hadhara"Nilishangazwa na uongo wa Spika Makinda bungeni
akieleza kuwa Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe alisimama kwa kifungu 53
(c)
wakati alisimama kwa kutumia kifungu 51(c) akipendekeza kuondolewa bungeni kwa hoja binafsi ya Mnyika"alisema Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk Willibrod Slaa.
Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alisema kwamba namna mijadala ya Bunge inavyoendeshwa, namna Spika anavyobeba ajenda za Serikali katika kujenga Bunge kibogoyo na namna anavyofanya maamuzi kwa kukurupuka, inahitaji hatua za kuokoa misingi ya uwajibikaji wa nchi.
"Ni lazima Spika wa Bunge adhibitiwe kwa kuondolewa katika nafasi hiyo haraka iwezekanavyo. Spika lazima ajue kwamba Mamlaka yapo kwa wananchi na yeye ni msimamizi tu wa vikao vya Baraza la wananchi liitwalo Bunge. Anna Makinda lazima adhibitiwe, vinginevyo nchi itaumia"alisema Zitto.
Naye Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alisema kwamba, kazi yao ni kufanya kile walichotumwa na watanzania, na baada ya hapo wanarudisha majibu ya kazi zao, "Sisi kazi yetu ni kutekeleza kile mlichotuagiza tukakifanye na baada ya hapo tunarudisha majibu kwenu, haya ndiyo majibu ya kazi tuliyoifanya katika Bunge hili, mtaamua wenyewe cha kufany kwani tulisema kwamba tutakuja kumshtaki kwenu na tumefanya hivyo, sasa zamu yenu kutoa hukumu juu yao"alisema Mbowe
No comments:
Post a Comment