Wednesday, February 6, 2013

KESI YA UBAKAJI YAANZA KUSIKILIZWA INDIA



HII NI KWA TAARIFA YAKO TU!



Kesi ya watu watano wanaotuhumiwa kumbaka na kumuua mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini India Desemba mwaka jana imeanza kusikilizwa. Rafiki wa mwanamke huyo, ambaye ni mhandisi wa komputa mwenye umri wa miaka 28, alitoa ushahidi katika kesi iliyosikilizwa kwa siri, na kuwatambua watuhumiwa hao na basi ambamo uhalifu huo ulitendeka. Inadaiwa kuwa wanaume sita walimshambulia yeye na mwanamke wakiwa ndani ya basi wakirejea nyumbani. Mwanamke alibakwa mfululizo na kuteswa kwa kutumia nyundo, na alifariki wikimbili baadaye kutokana na majeraha. Tukio hilo lilisababisha maandamano ya nchi nzima, na mjadala juu ya namna wanawake wanavyotendewa nchini India. Siku ya Jumapili, India ilianzisha adhabu kali dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia--- kwa kuweka kifungo kisichopungua miaka 20 kwa ubakaji, na adhabu ya kifo kama ubakaji huo ulisababisha kifo. Mtuhumiwa wa sita anashtakiwa tofauti kwa kuwa yeye ni mtoto.

 

No comments:

Post a Comment