Monday, February 25, 2013
kauli ya Lowassa
Dar- es -Salaam
SERIKALI imechukuwa maamuzi magumu ya kuunda tume ya kuchunguza sababu za wanafunzi wengi kufeli mitihani ya kidato cha nne,serikali imechukuwa hatua hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Waziri Mkuu aliyejiuzuri Edward Lowassa kuitaka serikali ichukue hatua hiyo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari hivi karibu Lowassa alidai kwamba tukio la kufeli kwa wanafunzi mwaka huu ni tukio la kushangaza na fedheha kwa taifa, serikali haipaswi kulifumbia macho.
Kauli hiyo ya Lowassa imemfanya Waziri mkuu, Mizengo Pinda atangaze kuwa ameunda tume itakayochunguza sababu za idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha nne kuvurunda katika matokeo ya mtihani huo yaliyotangazwa hivi karibuni.
Katika matokeo hayo ambayo yanatajwa kuwa mabovu kuliko yoyote yaliyowahi kutokea katika historia ya Tanzania, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo walipata daraja sifuri.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo alisema kuwa tume hiyo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo, ambapo itajumuisha Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi.
Lyimo aliwataja wadau wengine watakaohusika katika uchunguzi huo kuwa ni kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa)
“Tume hiyo itahusisha asasi zisizo za kiserikali (NGOs), zinazojishughulisha na masuala ya elimu. Wazazi, walezi na wananchi wote kwa jumla watoe ushirikiano kwa tume, ili ifanye kazi kwa ufanisi,” alisema Lyimo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment