Monday, February 18, 2013

R.I.P PADRE EVARISTI MUSHI PUMZIKA KWA AMANI BABA!


Gari ya padre Evaristi Mushi, baada ya tukio ndivyo linavyoonekana, watanzania tunakwenda wapi? lipi alilokosa padre huyo lililokosa msamaha?

Baada ya padre Evaristi kupigwa risasi kichwani, gari iliacha njia na kuuvaa ukuta wa nyumba hiyo hapo.
Watu wakishuhudia gari ilokua na padre Evaristi! nini kimejificha nyuma ya kifo chake?
Waziri Dkt Nchimbi (wa pili kushoto) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud na maafisa wengine walipotembelea eneo la tukio
 Mpakwa mafuta wa Mungu Padre Evaristi Mushi baada ya kurekebishwa eneo zilikoingilia risasi 3. pumzika kwa amani baba, tunasubiri kusikia sababu zilizoletelea kifo chako baba.

No comments:

Post a Comment