Monday, February 4, 2013

WASHIRIKI WA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 WASHIRIKI KUFANYA USAFI PAMOJA NA MEYA WA MANISPAA YA ILALA MH. JERRY SLAA, KATIKA ENEO LA FUKWE ZA AGHA KHAN JIJINI DAR ES SALAAM


Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa wanafanya usafi pamoja na Meya wa Manispaa ya  Ilala Muheshimiwa Jerry Slaa.

Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika picha ya Pamoja na Muheshimiwa Meya wa Ilala Jerry Slaa.
Kazi na dawa! kazi na tabasamu.
Pamoja na mheshimiwa Jerry picha ya pamoja!
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa wanafurahia baada ya kumaliza Zoezi la kufanya usafi katika Fukwe ya Bahari ya Hindi .

Washiriki 40  wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka mikoa yote na vyuo vikuu  waliopo katika kambi ya Taifa Ikondolelo Lodge  wakijiandaa na fainali za Taifa zitakazo  fanyika Tarehe 16.02.2013  Dar Live Mbagala. Leo wameshiriki katika zoezi la kusafisha ufukwe wa Bahari pamoja na Meya wa Manispaa ya Ilala Muheshimiwa Jerry Slaa.

Tamasha hilo maalum la kutunza na kujali Mazingira pamoja kuonesha umuhimu wa mazingira liliandaliwa na Shirika la Nipe Fagio ambalo limejikita katika mambo kusaidia jamii pamoja na Mazingira.


Katika Tamasha hilo ambapo Viongozi mbalimbali wa Serikali, pamoja na wananchi mbalimbali walihudhulia na kufanya usafi huo kuanzia saa moja asubuhi mpaka sa Nne kamili asubuhi, zoezi lilienda vizuri ambapo Warembo wa Miss Utalii Tanzania walishiriki kikamilifu na walionesha mfano mzuri kwa kuchapa kazi zaidi ya kukusanya taka taka hizo

No comments:

Post a Comment