Kumekuwa na matukio kadhaa katika Soka la Bongo amba katika Uwanja wa Taifa, ambapo baadhi ya matukio hayo huwa ni ya hatari na mengine huwa ni ya uzembe wa askari wanaokuwa wakilinda usalama, ambao wengi wao huwa wamenogewa na kuangalia soka zaidi kuliko kulinda usalama uwanjani hapo.
Wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya timu ya Taifa Taifa Stars na Brazil, kuna tukio la shabiki mmoja aliyewahi kuruka kutoka jukwaani na kuingia katikati ya uwanja kwa lengo la kumkumbatia mchezaji wa timu ya Brazil, KAKA, ambaye aliweza kuruka kutoka jukwaani hadi kuingia katikati ya uwanja huku askari wakipigwa na butwaa, hiyo yote ilikuwa ni kwa sababu hawakuwa makini kulinda usalama bali walikuwa makini katika kuchek soka zaidi.
Na matukio mengine kadhaa yaliyowahi kutokea, jingine ni la huyu mlemavu pichani, ambaye katika mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga na Tanzania Prisons ni huyu huyu ambaye alichomoka alikokuwa na kujaribu kuingia uwanjani ili kumkumbatia Mbuyu Twite, ambapo askari pia walishtukia akiwa tayari anakaribia kukanyaga nyasi za uwanja huo karibu kabisa na goli.
Askari hao walimbeba na kumtoa nje, wakati wakijaribu kutaka kumpakia katika gari lao mlemavu huyo alitoa mpya kwa kuvua nguo zote na kubaki mtupu jambo lililowafanya askari hao kushindwa kumdhibiti na kuamua kumuachia huru na kuondoka zake.
Lakini tena ni mlemavu huyu huyu, ambaye hivi majuzi katika mechi ya Yanga na Azam, aliruka uzio kutoka Jukwaa la Mashabiki wa Yanga na kutua katika Jukwaa la VIP ambalo hukaa waandishi wa habari, pamoja na walio na tiketi za VIP na kuanza kumvamia mwandishi wa habari mmoja wa Redio, aliyejulikana kwa jina la Sultan Sikilo, aliyekuwa amevalia Tisheti nyekundu huku akimtaka kuvua tisheti hiyo ama kuhama mahala hapo.
Eneo hilo ni maalum kwa wanahabari na wala halihusiani na mashabiki wa timu fulani kwani wanaokaa eneo hilo wenye tiketi za VIP ni wale wenye ustaarab ambapo unaweza kukuta ni mashabiki wa timu zote wakiwa eneo hilo na bila kuzuliana.
Cha kushangaza zaidi ni kwama eneo hilo walikuwapoa askari lakini, mlemavu huyo aliweza kuruka kutoka upande wa pili wa jukwaa la mashabiki wa Yanga na kutua upande VIP na kuanzisha vurugu hizo na ndipo askari waliokuwapo eneo hilo wanashituka na kuanza kumdhibiti wakati tayari alikwisha mvamia mwandishi huyo ana kama angekuwa na silaha yeyote tayari angekwisha mzulu mwandishi huyo.
Pamoja na sakata hilo kuingiliwa na wastaarabu waliokuwa eneo hilo lakini bado mlemavu huyo aliendelea kushikilia msimamo wake wa kuondolewa mwandishi huyo katika eneo hilo ama kuvua tisheti hiyo, jambo ambalo liliwafanya askari hao kumuondoa mwandishi huyo na kumpeleka upande wa pili.
USHAURI BINAFSI:- Mtandao huu unawaomba wahusika kusimamia ipasavyo amani na usala katika viwanja vyetu vya michezo na ikibidi waige mfano wa askari wa nchi za wenzetu, ambao wao hufanya kazi iliyowapeleka uwanjani tu, kwa kugeuka na kutazama jukwaani na si kuangalia upande wa uwanjani na kunogewa na soka na kujisahau kulinda usalama, hadi linapotokea jambo ndiyo wanashituka.
Askari hao wakijaribu kumdhibiti mlemavu huyo, kwa jitahidi kumsihi mwandishi Sultan Sikilo, kuondoka katika eneo hilo.
Mlemavu huyo, akijitutumua kurusha konde ili kutaka kumtwanga Sultan.
Askari wakimuondoa Sultani katika eneo hilo.
Hapa napo ni wachezaji wa Azam Fc, waliokuwa wakimzonga mwamuzi wa mchezo huo kutaka kumpa kipondo kwa madai ya kutochezesha Fea.
Askari wakiwaondoa waamuzi uwanjani chini ya ulinzi mkali.
No comments:
Post a Comment