Wednesday, July 25, 2012

Piga picha Ashuhudia ,Bahari na Maajabu Yake!!!!!!


                       Alichoshuhudia baasa ya kupiga picha!!!! Shark na wanawe mbavuni!!!!

Shawn Heinrichs ndiye aliyepiga picha hiyo katika pwani ya Mexico ,ambaye kitaaluma ni mzamiaji! Mpiga picha na mpiga picha za filamu, ameeleza habari nyingi za kushangaza baharini lakini kwa shark ambao ni samaki wakubwa duniani lakini kwa huyo!? Amezima sigara , na akaamua kushare na jamii ya facebook!
Shawn anasema kua siku aliyopiga picha hiyo! Bahari ilikua tulivu mno! Na Sharks wote walikua wazi wazi ,na mara nikaona bonge la shark likikatiza jirani na boti yetu ,nikarudi nyuma kidogo na kusubiri, na picha hii niliyoipata inahitaji utaalamu sana wa kiufundi! Wa kujua namna ya upigaji picha na uzoefu nao unasaidia! Japokua watu wengi hawaamini kama ni shark wa ukweli,kwani unapaswa uviweke sawa vitu vilivyo juu na chini ya maji sababu ni changamoto kubwa sana kuvitenganisha
wapiga picha ambao ni watanzania wenzangu! Mnapenda adventure? Naomba picha zenu nitupiemo humu bloguni!!!

Friday, July 20, 2012

Shughuli ya kutafuta maiti Zanzibar


                                                                              Ramani


                                              Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya M.  Kikwete

Shughuli ya kutafuta maiti kwenye ajali ya meli iliyozama nchini Zanzibar ilianza leo mapema huku watu miamoja wakiwa bado hawajapatikana baada meli iliyokuwa inaelekea kisiwani Zanziabr kuzama eneo la Chumbe.


                                                 Meli ya Star Gate ikizama

Meli hiyo ilitoka Dar Es Salam jana mcahan kuelekea kisiwani ikiwa imebeba watu miambili tisini.Hadi kufikia sasa maiti 31 wamepatikana huku watu zaidi ya 150 wakiokolewa.
Msemaji wa polisi , Zanzibar aliambia shirika la habari la AFP kuwa kwa sasa kuna hofu ya kutopatikana manusura wowote waliokuwa katika meli hiyo ya MV Skagit
"shughuli ya kuwatafuta manusura na maiti inaendelea lakini kwa sasa ni vigumu kwa kweli kupata manusura." alinukuliwa akisema msemamji huyo wa polisi.
Siku tatu za maombolezo
Manusura walisema kuwa walihofia baadhi ya wasafiri wa meli hiyo walikwama katika meli ilipobiruka na kuanza kuzama kwa sababu ya upepo mkali.
Ali Mohamed Shein, rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, ametangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa.Meli hiyo iliondoka Dar es Salaam saa sita mchana kwa saa za Afrika Mashariki hapo jana ikiwa inelekea kisiwani Zanzibar.


                                                                 Dr Shein Rais wa Zanzibar

Hamza Kabelwa, afisaa mkuu mtendaji katika idara ya hali ya hewa nchini Tranzania, aliambia BBC kuwa onyo lilitolewa kuhusu hali mbaya ya hewa na hivyo vyombo vya majini havikupaswa kufanya safari zozote.
Waziri wa usafiri wa Zanzibar aliambia waandishi wa habari kuwa watalii wawili kutoka Ulaya ni miongoni mwa waliofariki.Shughuli za uokozi zilisitishwa jana jioni kwa sababu ya dhoruba kali ya upepo.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salama,Hassan Mhelela aliambia BBC kuwa jamaa wengi wa watu waliokuwa kwenye meli hiyo walikuwa na wasiwasi na walikuwa wanajipanga kutumia ndege kwenda Zanzibar kutafuta jamaa zao.


Kivukio hicho kati ya Dar es Salaam na Zanzibar hutumiwa sana na wenyeji pamoja na watalii
Mwezi Septemba mwaka jana, takriban watu 200 walifariki baada ya meli iliyokuwa imejaza watu 800 pamoja na mizigo, kuzama huko Zanzibar.


Wednesday, July 18, 2012

Drake Anamiliki Mjengo Mpya Na Hii ni Sehemu


Rapper mwenye hit zinazouza mbaya, ni kama anauishi ule usemi usemao unaishi mara moja tu! Ameangusha dola milioni 8 kwa kununua bangaloo huko Los Angeles,na kufanya ndoto zake kua kweli.





Mjengo huo wa ajabu wa Drake una futi 7,444  na uko katika heka tatu katika vilima vilivyojificha imemgharimu kama dola milioni 7.7, na mjengo huo una kila kitu ndani yake  na unaendana na gharama yake, ndani kuna mabafu kama tisa  ,vyumba vya kulala saba kuna home theatre,kiwanja cha tennesi na volleyball na kuna pool kali mno! Kama haitoshi! Drake anamiliki maporomoko ya maji, kuna sehemu ya pool ina grotto na baa ya majimaji


                                                    bar! yenye kila aina ya wines!!!!!!

Kama uonavyo si rahisi kuamini kijana wa miaka 25 tu kumiliki Mansion kama hiyo na kuiita nyumbani, lakini ni poa! Kilele cha mafanikio.

                                          Water falls pool  anayomiliki Drake!


Drake anajua kula na wakati, Mansion hiyo mnamo mwaka 2009 ilikua inagharimu  kiasi cha dola 27 milioni, na baada ya bei kushuka hadi dola milioni 9.95 na kupungua tena naye akamudu kuinunua akahamia!





        ukitoka katika poll ya maporomoko ya maji unafuata mkondo unaokuleta katika grotto.


Kwa sasa katika vilima hivyo vilivyofichika nyumba zake si za rahisi huanzia dola 1.2 hadi dola 13 milioni na ma celeb ambao hununua,kuuza,kupangisha wamo akina Britney Spears, John Mayer, Melissa Etheridge, Lisa Marie Presley, Ozzy and Sharon Osbourne,na  the Kardashian-Jenner ndo majirani wa Drake!


                                                                    Theatre ya Drake

Mzee Mandela Atimiza Miaka 94 leo



                      bango la kum wish mzee Madiba anapotimiza miaka 94 ya kuzaliwa leo.





Rais mstaafu wa Africa Kusini, Nelson Rholilla Madiba Mandela, leo hii anaadhimisha miaka 94 ya kuzaliwa kwake.Mjukuu wake aitwae NDILEKA , ameeleza kua sherehe za maadhimisho hayo zinatarajiwa kua katika jiji la JOHANNESBURGE, Pamoja na maonesho ya picha za Rais huyo mstaafu yanayoendelea.  



Rais huyo mstaafu, aliamua kustaafu kiukweli kwa shughuli zake zote  za kisiasa na muda wake mwingi anautumia akiwa na familia yake.


            baba Mandela akiwa na watoto na wajukuu

Tuesday, July 17, 2012

Sylvester Stalone afiwa na Mwanawe



Sage Stallone  alikua katika wakati muhimu sana katika maisha yake, kabla ya habari mbaya za kushtusha na hiyo ndo taarifa kutoka kwa mwanasheria wake George Braunstein wakati akiiambia NBC  jijijini Los Angeles
 Sage ambaye ni mtengeneza filamu ni motto wa Sylvester Stallone kwa mke wake wa kwanza Sasha Czak  na Sylvester anasema mwanawe alikua katika afya njema na mshawasha wa ndoa yake ulikua juu na alikua akifanya kazi nyingi za kutengeneza filamu akiifikiria ndoa yake ingawa mchumba wake hajajulikana
Ndani ya nyumba yake kulikutwa karatasi kadhaa za ununzi wa dawa kwa kidhungu kama prescription na alikutwa na chupa ya dawa ,na mwanasheria wake anasema bwana Braunstein anakana kua Sage alikufa kwa kuzidiwa na kiwango kikubwa cha dawa wakati akijaribu kujiua  yeye anakataa
Chanzo cha kifo cha kijana huyo kitachukua miezi kadhaa kuking’amua baada ya uchunguzi uchunguzi wa kitabibu utatoka baada ya wiki sita ili kung’amua kama kuna sumu yoyote alokula hiyo ni kauli ya  spokeswoman for the Los Angeles Department of Coroner  wakati akiiambia  NBC Los Angeles.
Wataalamu wa mambo ya kitabibu wanaeleza kua hakuna jaribio lolote la kutaka kujiua wakati walipouchukua mwili wa Sage nyumbani kwake katika vilima vya Hollywood na Sage hakuacha kikaratasi chochote cha ujumbe kabla ya kifo


                                                            baba na mwana
Mtoto huyo mkubwa wa Sylvester Stallone Sage alionekana katika filamu za  Rocky V, Daylight na  Chaos,na amesha direct the 2006 short film Vic.
Kutokana na kifo hicho cha Sage Sylvester Stallone amehamanika na mwenye huzuni nyingi na anamhurumia sana mama yake Sage, Sasha  na anafikiria namna anavyojisikia na anamuelezea Sage kama kijana aliyekua na kipaji cha ajabu na kijana mdogo wa kuajabisha na mwema wakati wote wa maisha yake na atamkumbuka milele.


                                                          Sylvester,Sasha na Sage

Thursday, July 12, 2012

Unawajua Kigoma All Stars?



                                                         Mwana Kigoma Zitto Kabwe
Kigoma All Stars walioimba wimbo -Leka Dutigite hawa hapa  -Abdu kiba, Baba Levo, Banana Zorro, Chege, Diamond, Linex, Makomando, Mwasiti, Ommy dimpoz, Queen Darling, Rachel wakiwa na Mhe. Zitto Kabwe
Hawa si wakwanza kuunda umoja wao ila walitofautiana kwa mantiki, Kigoma All Stars wao sabau yao wanatoka Kigoma! Baaaaasi lakini mkusanyiko kama huu ulikuwepo , mnamo mwaka 1985 ulitungwa wimbo wa WE ARE THE WORLD,ambao uliandikwa na nguli wawili ambao mmoja isivyo bahati amefariki dunia, namzungumzia Michael Jackson ambaye alishirikiana na Lionel Richie , producer alikua Quincy Jones,waliotia sauti walikua wanamuziki maarufu na mashuhuri kama ilivyo kwa Kigoma all stars sasa US FOR AFRICA lengo lilikua ni kuchangisha fedha kuwasaidia wa Ethiopia ambao walikumbwa na mafuriko ambayo yalikua ya kihistoria!Hiyo hapo

                        


Kigoma All Stars!
      


                    

                            Kigoma All Stars promo!

Mwaka huo huo wa 1985 hapa Tanzania wakati wa utawala wa Al haji Ally Hassan Mwinyi, alipokua na kampeni ya kuondo uvivu,uzembe na uzururaji makazini almaarufu ka FAGIO LA CHUMA!
Walijikusanya wanamuziki kibao, akiwemo Zahiri Zoro,na Mzee Gurumo na wengineo wakaimba juu ya kauli mbiu hiyo, si kwa hilo tu alipokufa Raisi wa Msumbiji Samora Mozes Machel walikusanyika tena na kuimba, hio haitoshi katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru Tanzania walikusanyika tena na kuimba.

Historia ikajirudia tena pale ambapo msanii wa Filamu maarufu kama Sajuki, alipoumwa sana wasamaria wema  walijikusanya kumchangia na wasanii wakafanya uhamasishaji na kutoa kitu kinachoitwa MBONI YANGU. WHA NEX! TIME WILL TELL, au siyo.

Wednesday, July 11, 2012

Kenge wa kipekee




  kakupa bonge ya swagger!huyu ni kenge!anatokea Mwanza tu hapo! Mungu ana mambo! dah kampambaje?kwa jamii hii mwanaume ndo huwa amepambwa namna hii, naamini nia ni kuvutia mademu.na hata alipokua akipigwa picha alipose kama spiderman mwenyewe!Mungu kaumba sifa na utukufu ni kwako baba Muumba.

kenge  huyo kutoka Mwanza aliyepelekwa katika eneo la Agama, mwenye asili  Africa na kwa kawaida huishi katika makundi na dume moja ndo huongoza kundi hilo na kwa asili hua ana rangi kama huyu!
Mpiga picha wa picha hiiCassio Lopes   alikua na raha isiyo elezeka na kusema huyo ni mmoja wa wanyama ambaye hajawahi kumwona tangu amezaliwa na mnyama aliyepakwa rangi nzuri namna hiyo! Na anafanana mno na spiderman kuanzia kifuani,mabega na miguu na anaonekana kama amevaa suti ya spiderman wakati alipokua akitambaa kwenye mwamba




                                   Kuna kufanana flan na spider man siyo? tazama kwa makini.




huyo kaka Cassio Lopes  ndiye aliyepiga picha hiyo, alikua Kenya kwa holiday! akiwa na mkewe  Alessandra

Picha hiyo ya Kenge ilipigwa wakati mpiga picha huyu  Cassio Lopes alipokua katika  Masai Mara National Park nchini Kenya akiwa na mkewe Alessandra.Cassio ana umri wa miaka 38 raia wa Sao Paulo, Brazil,na akiwa katika katika kazi zake za upigaji picha ,mchana mmoja waliamua kupumzika karibu na mto  Rongai.kulikua na ukame wakati huo, na tuliambiwa kua wakati wa asubuhi chui huonekana karibu ya hapo hivyo, hivyo tukaamua kupoteza muda ili kuwashuhudia chui!wakichomoza mtoni.
Baada ya muda mrefu bila kuwaona chui ,tukaanza kuangalia vitu vingine na mkewe ndiye aliyekua wa kwanza kumwona kenge huyo akiota jua juu ya mwamba jirani na mto Rongai.
Hii ni mara yetu ya kwanza kuona mnyama kama huyo japokua tumekwisha wahi kuja Africa mara kadhaa huko nyuma ,tulichanganyikiwa kwa rangi nzuri zakenge!na kitu kibaya zaidi mara tu baada ya kuona mwanga wa flash ya kamera  kenge huyo aliishia zake  miambani.
Na Cassio anamuelezea kienge huyo kwa tabia kwamba ni mwenye aibu mno kuliko hata Spiderman  mwenyewe na Cassio anaamini kua kenge  huyo aliwaletea  bahati kwani baada ya kuishia miambani ndipo  walianza kuwaona chui wakijitokeza! Ambao lilikua lengo letu hapo Mwanzo!

kwa kawaida huonekana hivi!


huyu amejitwalia rangi za Leopard!


walichokua wanakitafuta!

Tuesday, July 10, 2012

Wabunge Wa Wenzetu Hewani


Mambo hayo! Wakati wabunge watanzania wao wameamua kuzogoa mjengoni na mahali hapo patukufu kufananishwa na soko la kariakoo, taifa la Jordan limeingia doa laa ajabu lisilotoka hata kwa jik na kusababisha waingie katika kitabu cha Guiness book of records!! Y? twende sawa sasa.
Mbunge Mohamed Shawabka anashikiliwa na wana usalama wa Jordani kwa jaribio la kutaka kumdhuru mbunge mwenziwe kwa bastola ndogo wakati wakiwa katika mahojiano ya live, katika kituo cha Television cha taifa la Jordan.
Mohamed Shawabka katikati ya kipindi hicho cha TALK SHOW alimtolea bastola bwana Mansour seif edine murad ambaye ni mdau wa masuala ya kisiasa baada ya kuambiwa kwamba yeye ni kibaraka wa rais  BASHAR AL ASSAD wa nchini SYRIA.
Hata hivyo kabla hajatoa bastola hiyo Bwana SHAWABKA alimrushia kiatu mpinzani  wake ambacho kilimkosa na kiatu hicho kikatua kwa mtangazazji wa talk show hiyo MOHAMED HABASHNA ambaye pamoja na  kuamulia ugomvi huo bila ya mafanikio yoyote akaona isiwe taabu akafunga mazungumzo hayo iliyokua ikitizamwa,na mandhari yake yalikua sege mnege na hakuna aliyejeruhiwa katika sakata hilo. ona hapo chini.





Friday, July 6, 2012

Malia Obama Atimiza Miaka 14


                                       Sasha akiwa na dada yake Malia na Mama yao!

Mtoto mkubwa wa Rais Barak Obama, Malia alisherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwake akiwa ikulu ya Marekani july 4 na muonekano wake kwasasa anaonekana kukua hasa na kama hiyo haitoshi!  anaonekana kufanana mno na mama yake kwa vitu vingi.


Malia Obama akiwa ndiye kifungua mimba wa Obama na Michelle alisherehekea birthday yake sambamba na siku ya uhuru wan chi yake Marekani.zawadi ambayo  First Lady Michelle ameitaja ni zawadi ya simu ya kiganjani lakini alipewa sharti na mama yake ,kusoma maelezo yahusuyo simu hiyo ili kuielewa na kujua ni simu ya namna gani.
Michelle na Obama walikubaliana kwa pamoja na kuamua Malia mwenye miaka 11, na Sasha mwenye miaka 11, hatatakiwa kuitumia simu hiyo mpaka wafikishe miaka 17! Hiyo wakaitupia katika ukurasa wa facebook, lakini je wataweza.?

Michelle  ali tweeted ujumbe maalumu katika twitter kwa motto wake huyo nauweka kama ulivyo!!!!!!! the big day: “Happy Fourth! What makes this day even more special is that it’s the day our first child was born. Happy birthday, Malia! We love you. –mo” habari ndo hiyo!
Michelle na binti yake kwa sasa wanafanana mno kuliko wakati mwingine wowote na urefu wa Malia kwa sasa ni inchi 5’11 sawa na urefu wa mama yake na Michelle anaeleza kua binti yake sasa walau ameamua kujiachia kimavazi na mabadiliko yake yanaonekana wazi kwani hata make up anatupia Malia!

Mbali hayo! Malia amekwisha onesha chembe chembe za kupenda mavazi na fashions  kama mama yake


                                                 Mama na Mwana, binti kajiachia!

Waisilamu kulinda makanisa Kenya



                                            matokeo ya mashambulizi
       
Viongozi wa kiisilamu nchini Kenya wamekubaliana kuunda makundi ya kutoa ulinzi kulinda makanisa kutokana na mashambulizi kama yaliyotokea kaskazini mwa Kenya siku ya Jumapili.
Watu kumi na watano waliuawa katika mashambulizi mawili dhidi ya makanisa mawili mjini Garissa karibu na mpaka wa Somalia.



                                                 kanisa target ya Al-Shabab

Eneo la mpakani mwa Kenya na Somalia limekumbwa na hali ya wasiwasi tangu Kenya ilipopeleka majeshi yake kupambana wanamgambo wa al-Shabab.Mkuu wa baraza la waisilamu nchini Kenya, Adan Wachu,aliambia BBC kuwa kitendo cha Jumapili kilikuwa cha ugaidi.
Waisilamu wanahisi kuwa kwa sababu wakristo ni wachache katika sehemu hiyo hakuna budi kuwalinda."Kuna watu huko nje wanaotaka kufanya kila wawezalo kufanya Kenya kama Nigeria." Alisema bwana Wachu, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la viongozi wa kidini nchini Kenya."
"Sisi hatutaruhusu kutokea ghasia za kidini nchini humu, yeyote aliye na nia ya kuchochea hali hiyo afahamu kuwa hatafaulu." aliongeza Wachu.Alisema kuwa sasa ni juu ya viongozi waisilamu mjini Garissa kupanga namna ambavyo makanisa thelathini yaliyo Garissa yatalindwa.


                                                    sehemu ya kundi la A-Shabab

Watu wengi wanaoishi ndani na kando ya mji wa Garissa ni wasomali na ambao ni waisilamu.Mwezi Oktoba mwaka jana wanajeshi waliingia nchini kupambana dhidi ya al-Shabab wanaotuhumiwa kufanya vitendo kadhaa vya utekaji nyara na kutatanisha usalama kwenye eneo la mpakani.
Lakini tangu hapo Al Shabaab limelaumiwa kwa kufanya msururu wa mashambulizi ya maguruneti katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.Viongozi wa kundi hilo, hawajajibu shutuma zozote za kufanya mashambulizi ya Garissa.

Korea Kuanza Uwindaji Wa Nyangumi


inawezekana kua huyu ni nyangumi mtoto anapelekwa kwenye uchunguzi.

Ikumbukwe kuwa Nyangumi ndiye mnyama mkubwa kuliko wote duniani.Haishangazi kuona nyangumi mkubwa zaidi ya huyo.Ni kitoweo kinachouzwa kwa bei mbaya Japan na nchi nyinginezo..

Jicho la nyangumi hilo!

Sasa basi, Korea ya Kusini imetangaza kua inataka kuwa inataka kuanza uwindaji wa nyangumi chini ya sheria inayoruhusu uvuvi wa nyangumi kwa minajili ya utafiti wa kisayansi, kama vile serikali ya Japan inavyofanya kwa sasa.
Serikali ya Korea ya Kusini,ilifichua hayo wakati wa mkutano wa kimataifa wa baraza linalosimamia na kulinda maslahi ya nyangumi nchini Panama,ambako walikua wakiwakilisha mipango yao kwa kamati ya sayansi ili kuchunguzwa.
Nyangumi hao watawindwa karibu na pwani ya Korea lakini haijulikani ni wangapi.Uvuvi wa nyangumi kwa minajili ya biashara imepigwa marufuku chini ya sheria za kimataifa,lakini uvuvi wa nyangumi  kwa minajili ya utafiti unaruhusiwa,hata kama nyama yake italiwa baadaye.
Korea ina historia ya ulaji wa nyama ya nyangumi kuliko eneo lolote ulimwenguni, na inakisiwa kwamba, utaratibu huo wa ulaji wa nyama ya nyangumi ulianza takriban miaka elfu nane iliyopita.!

Tuesday, July 3, 2012

Sekunde Chache Kabla ya Kifo


                                Ngadu na mamba! anamtupiamoooo!!!


Cheki nyoka alivyotanua mdomo kama mkono wa binaadamu, ndege kajikunyata zake! akija kutahamaki , kajaa mdomoni mwa nyoka huyo! hapo hatoki kwenye kumi na nane za nyoka.


chura akiwa amedakwa na nyoka eneo la mdomoni! na chura kwa ujasiri mkubwa, japo dakika za majeruhi kamshika nyoka shingoni! kwa vyovyote nyoka atashinda kwani atakua amesha muachia sumu! na hivyo atammeza kiulainiiiiiii.



Chura hana manusura hapo, kwani amebanwa kati kati ya mawe na kama uonavyo anashindwa hata kufurukuta! amesha vimba mwili na macho kumtoka, mwishowe ni kifo.



Papa akijiandaa kumla simbi! japokua avumaye baharini ni papa lakini wengine wapo,ingawa hawana msuli kama wake.

Hebu fikiria sekunde chache kabla ya kifo chako, eh naamini humjui  adui atakaye yachukua maisha yako kiukweli kabisa, na hapo Mungu aliweka siri kubwa sana juu ya sekunde chache kabla.



Ubaguzi wa Rangi Euro 2012 ni kwa Balotelli tu? why


                                            Picha hii inasema kila kitu

Picha hiyo hapo juu inaeleza maelfu ya maneno , itazame na unambie inamaanisha nini?halii kwasababu yuko kwenye timu ya Italia iliyopigwa na Spain! No! no! machozi hayo hayadanganyi.hii inaweza kua moja ya picha maarufu michezoni kwa mwaka huu wa 2012! Bila ya shaka yoyote.
Mario Baloteli, ni Mchezaji wa timu ya Italy na Mancity  ambaye amepata bahati ya kuandika historia, ya kuwa wa kwanza kuvaa jezi ya timu ya Italia Mario Maloteli a.k.a Super Mario, lakini pamoja na bahati hiyo ya pekee, ana bahati mbaya kwani hakubaliki na mashabiki wa taifa hilo kiasi cha kumchora  picha za namna kwa namna na kuchukuliwa kama ubaguzi wa rangi, hali amabyo inamkumbusha mengi maishani mwake.

                                moja ya dhihaka kwa Baloteli

 Hapa Mario akinyamazishwa na mchezaji mwenziwe alipokua akilia

                                     unaona taswira gani?

Na hi indo kauli yake dhidi ya kua mtu wa kwanza mweusi kuvaa jezi ya timu ya Italia, yeye kwa sasa ni muitalia ,ingawa anatokea katika nchi ya Ghana,nilitelekezwa na wazazi wangu, nikaasiliwa na watu wawili ambao kwangu ni sawa na malaika,ninataabika na ubaguzi wa rangi kila iitwapo leo,japokua mimi ni mtu wa kwanza mwezi kuvaa timu ya Italia,sina hasira,lakini uzoefu wa maisha yangu yananifanya nifanye mambo ndivyo sivyo kwa watu wengine,
Kwa msingi huo kabla hujaamua kunipinga,kwanza tafakari kwa makini ,hayo ni ya moyoni kutoka kwa Super Mario, kutokana na tabia zake , za  kitata sana , lakini pia hujiamini sana, mgomvi asiyehofu kitu, wa Itali  humfananisha Mario na nyani! Ana tabia ya kupenda sana mabibi na mengineyo.


Mwenyekiti Barclays ajiuzulu


                                                        Marcus Agius

Marcus Agius aliamua binafsi kujiuzulu kutokana kwa kile alichotaja katika taarifa yake ya kujiuzulu kama pigo kubwa linalotokana na kuharibiwa sifa kwa kampuni hiyo kwa sababu ya madai ya kuwalaghai wateja kupitia nyongeza haramu ya riba.
Wito umetolewa kuwa afisa mkuu mwandamizi wa kampuni hiyo, Bob Diamond ajiuzulu, kwa sababu alikuwa akisimamia uwekezaji wa benki hiyo wakati mpango ulipofanywa kulaghai wateja kupitia kwa riba inayotozwa katika benki hiyo.Hata hivyo wakurugenzi wa Barclays wameamua kuwa Bwana Diamond ataendelea kufanya kazi.
Kwa hivyo Bwana Agius, ambaye pia ni mwanachama wa Bodi, aliamua, huku akiungwa mkono na wenzake, kujitwika lawama zote zinazotokana na madhambi yanayokabili Benki ya Barclays na hasira yote waliyo nayo wenye hisa wa benki hiyo.
Mtu anayetazamiwa kuchukua mahali pake ni mkurugenzi mwingine, Sir Mike Rake, ambaye kwa sasa atalazimika kujiuzulu vyeo vyake vya kuwa mwenyekiti wa Easyjet na BT.
Naye Bwana Diamond hajajiondoa katika lawama bado kwani atahojiwa na Wabunge kuhusu mawasiliano ya siri ya mwaka wa 2008 kati yake na naibu wa Gavana wa Benki Kuu, Paul Tucker.
Meneja wa Barclays wanaamini kuwa ni katika mawasiliano hayo ambapo Benki Kuu ya Uingereza iliamuru Benki hiyo kudanganya kuhusiana na riba inayotozwa.
Hiyo haikuwa kweli lakini Bwana Diamond atalazimika kuwaeleza Wabunge anachokumbuka Bwana Tucker akimweleza wakati ule na kile ambacho baadaye aliwaeleza wafanyakazi wenzake.
Itakuwa aibu kubwa kwao iwapo yeye au Bwana Tucker watagunguliwa kwamba waliwashawishi wenzao kulaghai kupitia riba haramu.


Monday, July 2, 2012

Euro 2012


                                                Hii ni kwa mshindi Spain

Katika michezo timu ya Taifa ya Uhispania,imetunukiwa kuwa mabingwa wa Euro 2012 ambapo imeandika historia kwa maarifa ambayo siyo rahisi kuigwa, kwa kuifunga Italia magoli 4-0 katika fainali ya Euro 2012 usiku wa kuamkia leo mjini Kiev,Ukraine.
Licha ya mchezo wa Itali,vijana wa meneja wa Uhispania,VICENTE DEL BOSQUE walithibitisha kwamba kimataifa wanweza kujigamba wao ndio wenye mchezo bora zaidi duniani, kwa kuzingatia namna walivyoichezea timu ya Italia na kuwalazimisha kusalimu amri.

                                                              Vicente

David Silva aliifungia Uhispania bao la kwanza,kabla ya nusu ya kwanza ya mchezo kumalizika,mchezaji mpya wa Barcelona,JORDI ALBA aliandika bao la pili baada ya kukimbia na kumalizia kwa ustadi wa hali ya juu kabisa.

                                                  Jordi Alba

                                                                 David Silva

Ingawa Italia walikua na upungufu wa mchezaji mmoja, baada ya kumpoteza mchezaji wa zamu wa tatu THIAGO MOTTA baada ya kujeruhiwa,walicheza kwa bidii, lakini wataalamu wa kandanda kwa kujeruhiwa,walicheza kwa bidii,lakini wataalamu wa kandanda kwa upande wa kupokezana mpira,Uhispania, waliwahuzunisha sana.


                                                    Thiago Motta

FERNANDO TORRES aliingia kama mchezaji wa zamu na akafanikiwa kuubadilisha mchezo, na akaandika bao la tatu la Uhispania, kabla ya mwenzake katika club ya Chelsea, JUAN MATA, kuandika bao la nne na la mwisho la Italia, na ambalo bila shaka liliwavunja moyo kabisa mashabiki wote wa Italaia.

                        
                                                                Fernando Torres


mnyama Juan Mata alotia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Italia usiku wa kuamkia leo na kuwatawaza Spain kua mabingwa wa EURO 2012.