Thursday, July 12, 2012

Unawajua Kigoma All Stars?



                                                         Mwana Kigoma Zitto Kabwe
Kigoma All Stars walioimba wimbo -Leka Dutigite hawa hapa  -Abdu kiba, Baba Levo, Banana Zorro, Chege, Diamond, Linex, Makomando, Mwasiti, Ommy dimpoz, Queen Darling, Rachel wakiwa na Mhe. Zitto Kabwe
Hawa si wakwanza kuunda umoja wao ila walitofautiana kwa mantiki, Kigoma All Stars wao sabau yao wanatoka Kigoma! Baaaaasi lakini mkusanyiko kama huu ulikuwepo , mnamo mwaka 1985 ulitungwa wimbo wa WE ARE THE WORLD,ambao uliandikwa na nguli wawili ambao mmoja isivyo bahati amefariki dunia, namzungumzia Michael Jackson ambaye alishirikiana na Lionel Richie , producer alikua Quincy Jones,waliotia sauti walikua wanamuziki maarufu na mashuhuri kama ilivyo kwa Kigoma all stars sasa US FOR AFRICA lengo lilikua ni kuchangisha fedha kuwasaidia wa Ethiopia ambao walikumbwa na mafuriko ambayo yalikua ya kihistoria!Hiyo hapo

                        


Kigoma All Stars!
      


                    

                            Kigoma All Stars promo!

Mwaka huo huo wa 1985 hapa Tanzania wakati wa utawala wa Al haji Ally Hassan Mwinyi, alipokua na kampeni ya kuondo uvivu,uzembe na uzururaji makazini almaarufu ka FAGIO LA CHUMA!
Walijikusanya wanamuziki kibao, akiwemo Zahiri Zoro,na Mzee Gurumo na wengineo wakaimba juu ya kauli mbiu hiyo, si kwa hilo tu alipokufa Raisi wa Msumbiji Samora Mozes Machel walikusanyika tena na kuimba, hio haitoshi katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru Tanzania walikusanyika tena na kuimba.

Historia ikajirudia tena pale ambapo msanii wa Filamu maarufu kama Sajuki, alipoumwa sana wasamaria wema  walijikusanya kumchangia na wasanii wakafanya uhamasishaji na kutoa kitu kinachoitwa MBONI YANGU. WHA NEX! TIME WILL TELL, au siyo.

No comments:

Post a Comment