Tuesday, July 17, 2012

Sylvester Stalone afiwa na Mwanawe



Sage Stallone  alikua katika wakati muhimu sana katika maisha yake, kabla ya habari mbaya za kushtusha na hiyo ndo taarifa kutoka kwa mwanasheria wake George Braunstein wakati akiiambia NBC  jijijini Los Angeles
 Sage ambaye ni mtengeneza filamu ni motto wa Sylvester Stallone kwa mke wake wa kwanza Sasha Czak  na Sylvester anasema mwanawe alikua katika afya njema na mshawasha wa ndoa yake ulikua juu na alikua akifanya kazi nyingi za kutengeneza filamu akiifikiria ndoa yake ingawa mchumba wake hajajulikana
Ndani ya nyumba yake kulikutwa karatasi kadhaa za ununzi wa dawa kwa kidhungu kama prescription na alikutwa na chupa ya dawa ,na mwanasheria wake anasema bwana Braunstein anakana kua Sage alikufa kwa kuzidiwa na kiwango kikubwa cha dawa wakati akijaribu kujiua  yeye anakataa
Chanzo cha kifo cha kijana huyo kitachukua miezi kadhaa kuking’amua baada ya uchunguzi uchunguzi wa kitabibu utatoka baada ya wiki sita ili kung’amua kama kuna sumu yoyote alokula hiyo ni kauli ya  spokeswoman for the Los Angeles Department of Coroner  wakati akiiambia  NBC Los Angeles.
Wataalamu wa mambo ya kitabibu wanaeleza kua hakuna jaribio lolote la kutaka kujiua wakati walipouchukua mwili wa Sage nyumbani kwake katika vilima vya Hollywood na Sage hakuacha kikaratasi chochote cha ujumbe kabla ya kifo


                                                            baba na mwana
Mtoto huyo mkubwa wa Sylvester Stallone Sage alionekana katika filamu za  Rocky V, Daylight na  Chaos,na amesha direct the 2006 short film Vic.
Kutokana na kifo hicho cha Sage Sylvester Stallone amehamanika na mwenye huzuni nyingi na anamhurumia sana mama yake Sage, Sasha  na anafikiria namna anavyojisikia na anamuelezea Sage kama kijana aliyekua na kipaji cha ajabu na kijana mdogo wa kuajabisha na mwema wakati wote wa maisha yake na atamkumbuka milele.


                                                          Sylvester,Sasha na Sage

No comments:

Post a Comment