inawezekana kua huyu ni nyangumi mtoto anapelekwa kwenye uchunguzi.
Ikumbukwe kuwa Nyangumi ndiye mnyama mkubwa kuliko wote duniani.Haishangazi kuona nyangumi mkubwa zaidi ya huyo.Ni kitoweo kinachouzwa kwa bei mbaya Japan na nchi nyinginezo..
Jicho la nyangumi hilo!
Sasa basi, Korea ya Kusini imetangaza kua inataka kuwa inataka kuanza uwindaji wa nyangumi chini ya sheria inayoruhusu uvuvi wa nyangumi kwa minajili ya utafiti wa kisayansi, kama vile serikali ya Japan inavyofanya kwa sasa.
Serikali ya Korea ya Kusini,ilifichua hayo wakati wa mkutano wa kimataifa wa baraza linalosimamia na kulinda maslahi ya nyangumi nchini Panama,ambako walikua wakiwakilisha mipango yao kwa kamati ya sayansi ili kuchunguzwa.
Nyangumi hao watawindwa karibu na pwani ya Korea lakini haijulikani ni wangapi.Uvuvi wa nyangumi kwa minajili ya biashara imepigwa marufuku chini ya sheria za kimataifa,lakini uvuvi wa nyangumi kwa minajili ya utafiti unaruhusiwa,hata kama nyama yake italiwa baadaye.
Korea ina historia ya ulaji wa nyama ya nyangumi kuliko eneo lolote ulimwenguni, na inakisiwa kwamba, utaratibu huo wa ulaji wa nyama ya nyangumi ulianza takriban miaka elfu nane iliyopita.!
No comments:
Post a Comment