Monday, July 2, 2012

Euro 2012


                                                Hii ni kwa mshindi Spain

Katika michezo timu ya Taifa ya Uhispania,imetunukiwa kuwa mabingwa wa Euro 2012 ambapo imeandika historia kwa maarifa ambayo siyo rahisi kuigwa, kwa kuifunga Italia magoli 4-0 katika fainali ya Euro 2012 usiku wa kuamkia leo mjini Kiev,Ukraine.
Licha ya mchezo wa Itali,vijana wa meneja wa Uhispania,VICENTE DEL BOSQUE walithibitisha kwamba kimataifa wanweza kujigamba wao ndio wenye mchezo bora zaidi duniani, kwa kuzingatia namna walivyoichezea timu ya Italia na kuwalazimisha kusalimu amri.

                                                              Vicente

David Silva aliifungia Uhispania bao la kwanza,kabla ya nusu ya kwanza ya mchezo kumalizika,mchezaji mpya wa Barcelona,JORDI ALBA aliandika bao la pili baada ya kukimbia na kumalizia kwa ustadi wa hali ya juu kabisa.

                                                  Jordi Alba

                                                                 David Silva

Ingawa Italia walikua na upungufu wa mchezaji mmoja, baada ya kumpoteza mchezaji wa zamu wa tatu THIAGO MOTTA baada ya kujeruhiwa,walicheza kwa bidii, lakini wataalamu wa kandanda kwa kujeruhiwa,walicheza kwa bidii,lakini wataalamu wa kandanda kwa upande wa kupokezana mpira,Uhispania, waliwahuzunisha sana.


                                                    Thiago Motta

FERNANDO TORRES aliingia kama mchezaji wa zamu na akafanikiwa kuubadilisha mchezo, na akaandika bao la tatu la Uhispania, kabla ya mwenzake katika club ya Chelsea, JUAN MATA, kuandika bao la nne na la mwisho la Italia, na ambalo bila shaka liliwavunja moyo kabisa mashabiki wote wa Italaia.

                        
                                                                Fernando Torres


mnyama Juan Mata alotia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Italia usiku wa kuamkia leo na kuwatawaza Spain kua mabingwa wa EURO 2012.

No comments:

Post a Comment