Kasongo Mpinda Clayton
Wimbo wa nasononeka,wakati ukipigwa chumvi ilokua inatumika ni chumvi yam awe ndiyo iliyokua inatumika hapa Dar-es-Salaam. Pale lilipo daraja la Manzese leo hii almaarufu kama darajani, kulikua na msufi mkubwa sana, amabao ulikua kituo kikuu cha masi yaendayo mikoani,ambapo leo hii kituo kikuu kimefungiwa ndani ya kuta Ubungo Terminal.
Pale msufini viajana wa wakati huo wakati abiria wanasubiri mabasi ya mikoani vumbi mtindo mmoja,walikua wakicheza mpira barabarani, gari ikionekana kutoka ubungo maziwa vijana wanaacha kucheza mpira hadi gari ipite ndo wanaendelea tena.
Na kutoka Manzese Msufisini hadi Posta kulikua na kichaa mmoja tu aliyekua akijulikana kama Juma,peke yake lakini leo ni utitiri wa vichaa barabrani.kulikoni? maendeleo.yalikuwepo mabasi ya Moretco Morogoro, Retco ya Iringa naikumbukwe kwamba kila mji ulikua na shirika lake la mabasi, hapa nazungumzia miaka ya 1980- mpaka mwanzoni mwa miaka ya 90 ndipo yalipokufa kwa uchakavu,kushindwa kuyaendesha na ufisadi, leo hii si ajabu mmiliki wa basi wa miaka hiyo kukuomba wewe mia tano .
Wakati huo umoja wa familia ulikua very tight, mwanafunzi alikua akitoka kwa wazazi wake kwenda kwa mjomba alikua na uhakika wa ada,uniform na mazagazaga kibao, lakini leo hii ile ukiingia tu kwa mjomba unaulizwa unaondoka, na huondoki na chochote na hakuna umoja tena.
No comments:
Post a Comment